Maelezo ya jumla

Maumivu ya sikio moja au yote mawili na kushindwa kusikia mara nyingi hutokana na maambukizi kwenye sehemu ya kati ya sikio ‘’middle-ear infection’’. Unaweza kuwa na homa na kujihisi unaumwa mwili kwa ujumla. Wakati mwingine ngoma ya sikio inaweza kupasuka kwa sababu ya ongezeko la shinikizo. Baadae majimaji huanza kutoka sikioni. Maumivu ya sikio pia yanaweza kusababishwa na maambukizi kwenye sehemu ya nje ya sikio (hii inawapata zaidi watu wanaoogelea ‘’swimmers ear’’). Maambukizi haya yanaweza kuambatana na maambukizi kwenye koo, mianzi ya fuvu la kichwa au matatizo ya meno. Unaweza pia kupata maumivu ya sikio kama kamasi zimeziba masikio kwa sababu ya mafua, tukio la mzio au kama mgandamizo wa hewa kwenye sikio umebadilika ukiwa kwenye ndege.

Mwone dakatari kama

Panga kumwona daktari kama:

  • Una maumivu makali kwenye sikio na unapata homa au unatokwa na uchafu kwenye sikio

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe nyumbani kama una maumivu ya sikio

Wakati ukiendelea kufuatilia ushauri uliopewa na daktari, fanya mambo yafuatayo kupunguza au kutibu maumivu ya kawaida

  • Tumia dawa ya maumivu ili kupunguza karaha. Madawa kama ”acetaminophen” au ”ibuprofen” yatapunguza karaha na kupunguza pia homa kama una maambukizi sikioni
  • Unapotaka kulala, tumia mto ili kichwa kinyayuliwejuu, tumia mito kadhaa ili kupunguza shinikizo kwenye sehemu ya kati ya sikio ‘’middle ear’’
  • Kama maumivu ya sikio yamesababishwa na mafua, jaribu kutumia ‘’decongestants’’.
    • Hizi ni dawa ambazo zipo kwa mfuo wa ”spray” au matone na zinasaidia kufungua pua zilizozibwa na mafua. Zinafungua pia mianzi ya fuvu la kichwa ‘’sinuses’’ na sehemu ya kati ya sikio ‘’middle ear’’ kama una mafua au mzio
    • Usitumie ‘’decongestants’’ kwa zaidi ya siku 7 mfululizo. Ukiendelea kutumia dawa hizi kwa muda mrefu unaweza kuanza kupata tatizo tunaloita kitaalamu ‘’rebound effect’’.
    • Mtu mwenye tatizo hili anarudiwa na dalili za kuziba pua punde tu anapoacha kutumia dawa hizi, akiacha tu, pua zinaziba.
  • Weka joto kwenye sikio ili kupunguza maumivu
    • Unaweza kuchukua kitambaa kisafi, ukakiloweka kwenye maji ya moto , ukakikamua na kisha ukakishikilia kwenye sikio linalouma mpaka utakapoona kimepoa , kisha kipashe tena
    • Kama mbadala, unaweza kulaza sikio kwenye chupa ya maji, iliyowekwa maji ya moto
  • Kama ngome ya sikio ikipasuka, kunaweza kuwepo na majimaji au uchafu unatoka kwenye sikio. Kausha sikio kwa kitambaa na kisha panga kwenda kuonana na daktari

Mwone daktari kama una maumivu ya sikio na;

Panga kumwona daktari kama:

  • Kama dalili zinazidi kuongezeka au hazijaanza kupungua ndani ya masa 24 baada ya kuanza matibabu

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003046.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *