Maelezo ya jumla

Mba (dandruff) hazina madhara yoyote, lakini zinakera na zinaaibisha. Ukiwa na tatizo la hili, ngozi ya kichwa inakuwa inatoa seli nyingi zaidi zilizokufa zinazotakiwa kuondolewa. Seli hizi nyeupe kama vipande vya ukoko zinabakia kwenye nywele au mabega kama umevaa nguo yenye rangi nzito. Unaweza kuhisi ngozi ya kichwa inawasha na kuwa nyekundu. Kope, pua na hata paji la uso linaweza kuathirika pia.
Mara nyingi utakuta mba zinahusishwa na kuwepo kwa fangasi kichwani, au kuwepo kwa ugonjwa wa ngozi unaoitwa seborrheic dermatitis ambao unasababisha kuvimba kwa ngozi. Ugonjwa huu unasababisha ngozi kuwasha, kakamaa na kuwa kama gamba la nyoka. Wakati mwingine, kope za macho huathirika pia.
Tatizo hili huwaathiri zaidi wanaume na huzidi kuwa mbaya zaidi kama mgonjwa ana msongo wa mawazo, ugonjwa mwingine au kama anatumia aina fulani za bidhaa za kutunzia nywele.

Mba – unachoweza kufanya mwenyewe nyumbanimba

Ukifanya mambo yafuatayo, yatasaidia kuwaondoa. Lakini utahitaji kurudia kufanya hivi mara kadhaa, kwa sababu mba hujirudia rudia hata baada ya kupona.

  • Tafuta shampoo ambayo inaondoa mba ”antidandruff shampoo”. Osha nywele kwa kutumia maji ya uvuguvugu na sio ya moto. Sugua kwa shampoo mpaka kwenye ngozi. Iache kwa muda ili ifanye kazi – kwa kawaida inabidi uiache kwa dakika 3-5. Suuza nywele vizuri kabisa.
    • Shampoo za kupambana na Mba huondoa kabisa mba baada ya wiki kadhaa. Fuata maelekezo vizuri, bidhaa kutoka makapuni tofauti huwa na maelekezo tofauti
  • Endelea kutumia ”brand ya shampoo” ya kuwaondoa, ambayo unaona inakusaidia. Kama ukiona unaanza kuwashwa au kapata upele baada ya kuitumia, acha na kisha badili ili utumie nyingine yenye mchanganyiko tofauti.
  • Jaribu kuepuka kutumia bidhaa za nywele zenye pombe ndani (alcohol –based products). ”Sprays” zinasababisha ngozi ya kichwa kuwa kavu na gel au dyes za kubadili rangi nywele, zinaongeza harara na zinaweza kusababisha Mba kuongezeka zaidi.

Mba – tafuta msaada kama

Panga kuonana na daktari:

  • Kama unaona mba haziishi japo umekuwa ukitumia njia hizi zote nyumbani
  • Kama umepata muitikio mbaya  kwa moja ya shampoo ulizokuwa unatumia na unaona shida inaendelea
  • Kama ngozi ya kichwa imebadilika na kuwa na wekundu na unahisi maumivu sehemu sehemu za kichwa

Vyanzo

https://medlineplus.gov/dandruffcradlecapandotherscalpconditions.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *