Mfumo wa fahamu
Mfumo wa fahamu unawezesha mawasiliano ya sehemu moja ya mwili na nyingine
Mfumo wa fahamu umeundwa na ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu iliyosambaa mwili mzima.
Ndani ya viungo hivi kuna seli maalumu za mfumo wa fahamu zinazobeba jumbe tofauti tofauti na kuzisambaza haraka mwilini kama umeme.
Kazi za mwili, mjongeo wa misuli na utawanyaji wa taarifa mbalimbali, huogozwa na ubongo kwa kutuma taarifa mbalimbali kwenda sehemu mbalimbali za mwili na kwa kupokea taarifa kutoka sehemu mbalimbali za mwili kupitia mishipa ya fahamu.
Mfumo wa fahamu unaongoza maisha yetu.
Na, ukipata hitilafu, mambo yanaharibika kabisa; kifafa, kiharusi, kupooza n.k.
Unapaswa kulinda mfumo wa fahamu
- Jikinge na magonjwa
- Funga mkanda au vaa kofia ngumu (helmet) unapokuwa sehemu ya hatari
- kula mlo kamili
- Fanya mazoezi
- Usinywe pombe, usitumie madawa ya kulevya au kuvuta sigara
- Pata usingizi wa kutosha