Mfumo wa mkojo

Mfumo wa mkojo unafanya kazi ya kuchuja damu na kuondoa uchafu mwilini.

Kwa hali ya kawaida, mpaka lita 2 za mkojo hutengenezwa kwa siku.

Figo ni kiungo kinachofanya kazi ya kuchuja damu.

Damu huingia kwenye figo kwa kupitia mishipa ya ateri ya figo.

Ndani ya figo, uchafu na vitu mbalimbali huchujwa kutoka kwenye damu na kuingizwa kwenye mfumo wa mkojo.

Baadhi ya vitu vilivyochujwa na kuingia kwenye mfumo wa mkojo hufyonzwa tena kurudishwa kwenye damu na vingine kurudishwa kwenye mkojo.

Shughuli hii yenye hatua tatu, husafisha damu na kutengeneza mkojo.

Mkojo huondoka kutoka kwenye figo na kushuka chini kupitia mirija ya ureter mpaka kwenye kibofu.

Kadri kibofu kinavyojaa mkojo, taarifa kutoka kwenye ubongo kupitia mishipa ya fahamu husababisha misuli ya kibofu kukaza na kutoa mkojo nje.

Ni muhimu kukojoa ili kutoa uchafu mwilini

  • Kunywa maji ya kutosha
  • Punguza kiasi cha chumvi unayokula
  • Punguza kiasi cha kahawa unachokunywa
  • Kunywa maji zaidi wakati wa michezo au jua kali
  • Kojoa na jisafishe kila baada ya kushiriki ngono
  • Hakikisha unakojoa unapobanwa, usisubiri!
  • Mwone daktari kama unahisi unaumwa

Vyanzo

https://medlineplus.gov/kidneysandurinarysystem.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *