Mfumo wa uzazi
Mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanamme hufanya kazi pamoja kupata mtoto.
Mfumo wa mwanamke na mwanamme hujumuisha viungo vinavyotengeneza seli za uzazi, viungo vinavyotunza au kusafirisha seli za uzazi na viungo vya ziada vinavyosaidia na kuhakikisha mchakato huu unakwenda sawa.
Kwa mwanamme: tezi dume, korodani na uume
Kwa mwanamke: ovari, mirija ya uzazi, mji wa mimba, mlango wa mji wa mimba na uke.
Wakati wa uzazi, mbegu ya kiume na yai la mwanamke huungana ili kutengeneza yai lililorutubishwa.
Ujauzito ni matokeo ya mfululizo wa matukio.
Yai lililoutubishwa hujiotesha kwenye ukuta wa mji wa mimba na kukua kuwa mtoto
Mtoto aliyepatikana hubeba mchanganyiko wa chembe za urithi kutoka kwa mama na kwa baba pia.
Linda mfumo wako wa uzazi unapswa kulindwa
- Pata matibabu ya magonjwa ya ngono haraka
- Acha kuvuta sigara
- Dhibiti uzito wa mwili
- Punguza kunywa pombe
- Kula mlo wa afya