Mimba/ujauzito uliozidi umri wa kujifungua ni nini?

Mimba/ujauzito uliozidi umri wa kujifungua ni mimba iliyozidi wiki mbili baada ya siku tarajiwa ya kujifungua au baada ya wiki 40 za ujauzito. Moja kati ya mimba 10 mpaka 20 huzidi siku tarajiwa ya kujifungua.

Ni nini husababisha mimba/ujauzito uliozidi umri wa kujifungua?

Hakuna anyaejua baadhi ya wanawake kuwa na mimba/ujauzito uliozidi umri wa kujifungua. Hakuna sababu yoyote inayoonesha kuwa kuna kitu anachofanya mama kinachosababisha siku ya kujifungua kuchelewa. Kupata mtoto kutokana na mimba/ujauzito uliozidi umri wa kujifungua hakumaanishi kuwa mtoto ana tatizo lolote.

Je, kuwa na mimba/ujauzito uliozidi umri wa kujifungua kunaweza kunisababishia matatizo au mtoto wangu?

Kila ujauzito una hatari kiasi kwa mama na mtoto. Wanawake wenye mimba/ujauzito uliozidi umri wa kujifungua wana hatari zaidi ya kupata baadhi ya matatizo ukilinganisha na wanawake wanaojifungua karibu na wakati tarajiwa. Lakini hatari hizi sio kubwa sana.

Baadhi ya watoto wanaozaliwa baada ya mimba/ujauzito uliozidi umri hupata nyumonia na matatizo ya upumuaji. Baadhi ya wanawake hupata matatizo wakati wa kujifungua kwa sababu mtoto amekua mkubwa sana. Wakati mwingine wanawake wenye mimba/ujauzito uliozidi umri wanaweza kuhitajika kufanyiwa upasuaji ili kutoa mtoto.

Nifanye nini kama nisipojifungua sIku tarajiwa ya ujauzito wangu?

Hakuna jibu lililo sahihi kwa kila mtu kwa swali hili. Baadhi ya wanawake, baada ya kushauriana na daktari wanaamua kuanzishiwa uchungu uli wajifungue kama imekwishapita wiki moja baada ya siku tarajiwa. Uchungu unaanzishwa kwa kutumia dawa.

Baadhi ya wanawake, baada ya kushauriana na daktari wanaamua kusubiri mpaka uchungu uanze wenyewe. Lakini kama zitapita wiki tatu na bado haujapata uchungu, itamlazimu daktari kuanzisha uchungu kwa kutumia dawa.

Wanawake walioanzishiwa uchungu mapema wanapunguza uwezekano wa kufanyiwa upasuaji kuliko wanawake wanaoamua kusubiri uchungu uanze wenyewe.

Je, nitahitaji vipimo vyovyote maalumu?

Kama utaamua kuanzishiwa uchungu, yawezekana hautahitaji vipimo vyovyote maalumu. Kama ukiamua kusubiri uchungu uanze wenyewe, daktari anaweza kupendekeza ufanyiwe vipimo kadhaa. Daktari atatumia mashine kupima mapigo ya moyo wa mtoto wako. Anaweza pia kuhitaji ufanye kipimo/ kupiga picha ya ultrasound. Kipimo hiki kinamsaidia daktari kumwangalia mtoto na kuangalia kiwango cha majimaji anamoogelea mtoto akiwa tumboni. Baada ya kufanyiwa vipimo hivi, daktari anaweza kupendekeza uanzishwe uchungu au kusubiri.

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://www.news-medical.net/health/Pregnancy-over-40-weeks.aspx

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *