Maelezo ya jumla

Mmenyuko mkali wa mzio ni tatizo linalowapata baadhi ya watu. Baadhi ya watu hupatwa na hali hatari inayoweza kuhatarisha maisha baada ya kuumwa na mdudu, kula baadhi ya vyakula kama vile njugu au samaki, au kutumia madawa fulani. Mshtuko huu unaotokana na mmenyuko mkali au mjibizo mbaya wa mzio ‘’allergic reaction’’ huitwa ‘’anaphylactic shock’’ kitaalamu.
Dalili za ‘’anaphylactic shock’’ huanza dakika kadhaa baada ya kuumwa na mdudu au kula kitu ambacho ana mzio nacho, hii husababisha shinikizo la damu kushuka haraka sana na njia ya hewa kuanza kuziba kwa kasi. Dalili nyingine ni pamoja na kukorota; kuvimba macho na uso, midomo na ulimi; kupata vipele vyekundu vinavyosambaa mwili mzima; kutapia hewa kwa sababu hewa inashindwa kuingia ndani; na woga mkubwa. Kuna hatari kubwa ya kupata mshtuko na mtu kupoteza fahamu.

Mwone daktari

Mtu ambaye ana mmenyuko mkali au mjibizo mbaya unaotokana na mzio unaosababisha mshtuko ‘’anaphylactic shock’’ anahitaji msaada wa daktari haraka sana.

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe

Lengo lako kuu ni kumfikisha mgonjwa hospitalini haraka sana. Mtu mwenye mmenyuko unaotokana na mzio ‘’anaphylactic shock’’ anahitaji matibabu ya dharura, hii ni pamoja na kuchomwa sindano ya ‘’epinephrine (adrenaline). Watu ambao wana hatari ya kupata tatizo hili au wanajua kuwa wana mzio na chakula fulani hubeba na kutembea na sindano yenye epinephrine (adrenaline) ndani yake ili kujitibu wenyewe wanapopatwa na tatizo. Lakini wakati mwingine wanaweza kuhitaji msaada kuitumia. Wakati ukiendelea kusubiri usaidizi au ukiwa njiani kumpeleka hospitalini, mtulize na angalia upumuaji wake. Fuata hatua zifuatazo

  1. Omba msaada, tafuta usafiri ili kumuwahisha hospitalini. Muulize mgonjwa ni kitu gani kimesababisha mzio kwake. Ni vizuri kumuuliza wakati huu, itasaidia pia kumtuliza.
  2. Kama mgonjwa bado anajitambua/hajapoteza fahamu msaidi akae kitako, itasamsaidia kupumua vizuri. Usiwe na papara, tulia na mtulize pia. Mtie moyo kuendelea kuvuta hewa polepole na kwa nguvu.
  3. Kama mgonjwa ana sindano yenye epinephrine (adrenaline). Msaidie kuitafuta ili aitumie au unaweza kumchoma wewe mwenyewe kama unajua jinsi ya kuitumia.
  4. Tibu mshtuko ‘’shock’’ kama upo. Kama mgonjwa akipoteza fahamu lakini bado anapumua muweke alale upande upande ‘’recovery position’’ kama ilivyooneshwa kwenye picha.Mmenyuko mkali wa mzio
  • Hii itapunguza uwezekano wa kupaliwa na kurahisisha upumuaji. Endelea kufuatilia upumuaji na mapigo ya moyo mpaka utakapofika hospitalini au mpaka msaada wa kitabibu utakapokufikia.
  • Uwe tayari CPR kama mgonjwa ataacha kupumua. CPR ni utaratibu wa kukanda kifua na kupuliza pumzi puani ili kurejesha mzunguko wa damu na kupeleka hewa kwenye mapafu ya mgonjwa anaposhindwa kupumua na mapigo ya moyo kusimama.

Angalia pia: CPR – Makala hii inaandaliwa- itapatikana hapa baada ya muda kidogo

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000844.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *