Nawezaje kupunguza uwezekano wa mtoto kunywa sumu?
Matukio mengi ya watoto kula au kunywa sumu hutokea nyumbani. Unapaswa kuweka mbali na watoto kemikali za kusafishia na dawa zote. Dawa nyingi zinazotumiwa na watu wazima zinaweza kuwadhuru watoto au hata kuua, hata kama zimetumia kiwango kidogo tu. Usimeze au kunywa dawa zako mbele ya watoto wadogo, kwa sababu wanaweza kujaribu kuiga. Na usijaribu hata siku moja kuziita dawa zako ‘’pipi’’.
Nitunze vipi dawa zangu?
Hakikisha unafunga vizuri dawa na kuziweka kwenye kabati iliyofungwa kila baada ya kuzitumia. Hakikisha kuwa haziwezi kufunguliwa na mtoto.
Ni vizuri kutunza dawa zikiwa kwenye kifungashio chake cha mwanzo kilichoandikwa jina na namna ya kuitumia. Vifungashio vya dawa huwa na maelezo mazuri ya namna ya kuziweka salama. Kama unampatia mwanao dawa, fuata maelekezo kama ulivyoelekezwa na mtoa huduma ili usizidishe kiwango.
Wageni wanaweza kuja na dawa nyumbani kwako. Hakikisha hawaachi dawa kwenye mikoba au begi linaloweza kufikiwa na watoto. Mwombe mgeni aweke mbali dawa zake.
Nitajuaje kama mwanangu amekula sumu?
Kama mwanao ana dalili mpya au usizozielewa, inaweza kuwa ni kwa sababu amekula au kunywa sumu. Mwanao anaweza asiweze kukuangalia vizuri au anaweza kuonekana mchovu anayesinzia sinzia. Kunaweza kuwepo mchomo au kuungua kwenye midomo au mdomo, au harufu usiyoielewa inayotoka mdomoni. Unapaswa kushuku kuwa amekula sumu, ukikuta kifungashio cha dawa kilichokuwa na dawa kimefunguka au kama dawa zimemwagika.
Nifanye nini kama ninashuku kuwa mwanangu anamekula sumu
Kuwa mtulivu. Unaweza kumpigia daktari kama una namba yake. Kama mwanao anaonekana mgonjwa, anafanya matendo usiyoyaelewa, au kama anashindwa kuamka, ni vizuri kumpeleka haraka kituo cha afya. Kama unafahamua alichokula mwanao, chukua na kifungashio cha dawa uende nacho. Kama unajua aliyokunywa ni kemikali, fuata maelekezo yaliyo kwenye kifungashio kabla ya kumpeleka hospitali.
Katika kituo cha afya, unaweza kuombwa kutoa habari zifuatazo:
- Umri, urefu na uzito wa mwanao
- Matatizo yoyote aliyonayo mwanao
- Habari zozote unazozijua kuhusu sumu aliyokunywa nwanao -amekula, kunywa, kuvuta au kumwagikiwa na nini?
- Kama mwanao ametapika toka alipokula sumu
Fuata vizuri maelekezo uliyopewa na daktari
Angalizo
Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe.