Je, ninapaswa kuwa na wasiwasi kuwa mtoto atameza vidude?
Kumeza kitu – watoto wanaweza kumeza kitu bila kutarajia. Mara nyingi, kidude kitapita kwenye mfumo wa chakula na kutoka bila kusababisha matatizo yoyote. Wakati mwingine vitu vinaweza kukwama kwenye mfumo wa chakula na kusababisha matatizo makubwa.
Ninadhani mwanangu amemeza kitu. Nifanyeje?
Mpeleke mwanao kwa daktari kama unadhani amemeza betri au kitu chochote chenye ncha kali. Kama unadhani mwanao atakuwa amemeza kitu cha chuma (kama vile sarafu), ni vizuri kumwona daktari. Kama unadhani mtoto amemeza kitu kidogo kisicho na ncha kali (kama vile punji ya mkufu), hauhitaji kumpeleka kwa daktari haraka. Mpeleke kwa daktari kama mwanao akianza kupata dalili zifuatazo:
- Kutapika,
- utokwa mate mengi,
- Hali chakula,
- Maumivu ya tumbo,
- Anakohoa au
- Anakorota.
Wakati mwingine vitu vinawea kukwama kwenye koo / njia ya hew ana kusababisha matatizo. Mtoto anapaswa kupelekwa kwa daktari ndani ya masaa 24, hata kama anaoneka yuko sawa.
Daktari atafanya nini mtoto akimeza kitu?
Kitu cha kwanza atakachofanya daktari ni kujaribu kutambua ni nini mtoto amememza. Mtoto anaweza kuhitaji kupigwa picha ya eksirei ili daktari aone ni wapi kitu hicho kilipokwamia. Daktari anaweza kutumia vifaa maalumu ili kuhakikisha kitu hicho hakijakwama kwenye koo / njia ya hewa ya mwanao.
Kutegemea na wapi kilipo kitu hicho, daktari anaweza kujaribu kukiondoa au kukisukumia chini kuelekea tumboni. Vitu vingi vinavyofika tumboni hutoka vyenyewe kwenye kinyesi.
Daktari anaweza kuendelea kupiga picha kadhaa za eksirei kwa siku kadhaa ili kuhakikisha kitu hicho kinasogea kwenye mfumo wa chakula. Atakuambia uendelee kumuangalia kwa umakini kama atapata dalili fulani. Daktari anaweza pia kukuagiza ukague kinyesi cha mwanao kila mara ili kuona kama kitu hicho kimetoka.
Nifanyeje kumzuia mwanangu kumeza kitu /vitu?
Weka mbali na watoto vitu vidogo, hasa vyenye ncha kali na betri. Usimruhusu mwanao kuchezea midoli yenye sehemu ndogo ndogo zinazoweza kuchomoka akazimeza. Hakikisha kuwa, midoli ya watoto wakubwa yenye sehemu ndogo ndogo inawekwa mbali na watoto wadogo (midoli ya watoto wadogo hutofautiana na ya wakubwa)
Angalizo
Maelezo haya yanatoa muhtasari na yanaweza yasimguse kila mtu. Ongea na dakatri kuona kama ushauri huu unakufaa na ikibidi pata taarifa zaidi