Maelezo ya jumla

Kujikata kidogo, kujikwaruza mahali na kuchomwa na kijiti ni majeraha ya kawaida. Mkato kwa kawaida huvuja damu kwa muda mfupi tu. Mikwaruzo kwenye ngozi huvuja damu kidogo lakini inaweza kusababisha maumivu na kuruhusu vumbi na uchafu kukwama.

Mara nyingi utaweza kuhisi au kukiona kibanzi cha kijiti kilichokuchoma kwenye ngozi au ukucha, au unaweza kuvigundua baadae ukianza kuhisi maumivu, eneo kuwa la moto na jekundu kwa sababu ya maambukizi.

Japo majeraha haya ni madogo yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata pepopunda/tetanasi, maambukizi ambayo ni hatari na yanaweza kugharimu maisha. Kwa kawaida watu hupewa chanjo ya pepopunda wakiwa watoto lakini huhitaji kupewa chanjo ya nyongeza wanapokuwa wakubwa.

Kila baada ya kutibu jeraha lolote lililosababisha ngozi kuchanika, hakikisha kuwa umepata chanjo ya nyongeza ya pepopunda. Kama haujapata chanjo ndani ya miaka 10 au kama hauna uhakika ulipata lini chanjo, fika kituo cha afya upate chanjo.

Namna ya kutoa kijiti kilichokuchoma

Vijiti au vibanzi ”splinters” vingi vinaweza kuondolewa kwa urahisi. Lengo ni kutoa kijiti chote kama inawezekana na kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi. Vaa glavu kwanza kwa zinapatikana au nawa mikono vizuri.

  1. Osha eneo lililochomwa na  kijiti kwa sabuni na maji ya uvuguvugu na kisha pakaushe kwa kutumia kitambaa safi. Kama una ‘’tweezers’’ weka ncha zake juu ya moto ili kuua vijidudu vilivyopo. Subiri ‘’tweezers’’ zipoe kabla ya kuzitumia
  2. Bonyeza ngozi inayozunguka sehemu kibanzi kilipoingilia ili kusababisha ncha yake kujitokeza. Shika ncha ya kibanzi cha kijiti na kivute taratibu ili kukitoa. Hakikisha unakivuta katika usawa kilichoingilia ili kisivunjike.
  3. Bonyeza kidogo ngozi inayozunguka eneo lililoumia mpaka litoke damu kidogo. Damu inapotoka husaidia kuondoa uchafu wowote ambao unawea kuwa umebakia ndani ya jeraha. Osha eneo la jeraha kwa mara nyingine kwa kutumia maji ya uvuguvugu, pakaushe kwa kitambaa safi na pafunge kwa kutumia kitambaa safi au ‘’adhesive dressing’’
  4. Omba msaada wa kitabibu kama una kibanzi kikubwa kilichokuchoma na inakuwia vigumu kukitoa; kama eneo lililochomwa linaanza kuwa la moto, jekundu, limevimba na linauma; kama unaanza kupata homa; na/au kama hujapata chanjo au muda wa kupata chanjo ya nyongeza umefika au kama amesahau tarehe ya chanjo.

Namna ya kutibu kidonda kidogo au mkwaruzo kwenye ngozi

Lengo lako kubwa unapokuwa unatibu mkato mdogo, mkwaruzo au aina yoyote ya kidonda ni kuzuia damu isiendelee kutoka na kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi. Kabla ya kuanza vaa glavu kama zipo, au osha mikono vizuri.

  1. Dhibiti kuvuja kwa damu kwa kuweka gauze au kitambaa safi kwa nguvu (kundamiza) kwenye eneo la jeraha. Kama inawezekana, nyanyua eneo lenye jeraha juu kutoka usawa wa moyo, hii itasaidia kupunguza kiwango cha damu kinachosafiri kwenda kwenye jeraha. Mara nyingi mikato mingi huacha kuvuja damu baada ya dakika kadhaa.
  2. Suuza jeraha kwa kutumia maji safi yanayotiririka. Onoa uchafu kadri inavyowezekana. Tumia ‘’gauze’’ au kitambaa safi kusafisha eneo linalozunguka jeraha. Ondoa uchafu wowote uliojishikiza kwenye kidonda kwa kutumia kona/mkunjo wa kitambaa au ‘’gauze’’.
  3. Tumia kitambaa safi au ‘’gauze’’ kukausha. Funika jeraha kwa kutumia kitambaa safi au ‘’adhesive bandage’’. Usitumie pamba au bidhaa yoyote inayoweza kunatia kwenye kidonda.
  4. Tafuta msaada wa daktari kama jeraha /kidonda kinaachia, kimeachama au kama kimeingia ndani sana kuliko ulivyotegemea; kama hauwezi kuondoa mchanga au uchafu wote kutoka ndani ya jeraha; eneo la jeraha linaanza kuwa la moto, jekundu, kuvimba na kuuma; na/au kama muda wa kupata chanjo ya pepopunda umefika, haujawahi kupata chanjo au kama haukukbuki tarehe ya kupata chanjo.

Vyanzo

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *