Njia 9 za kupunguza kunywa pombe

Labda siku hizi umejikuta unakunywa pombe nyingi kuliko ilivyo kawaida yako. Kunywa pombe nyingi sana au mara nyingi sana kunaweza kuweka afya yako katika matatizo. Kunaweza pia kuharibu mahusiano yako na hata kazi yako.

Ni vizuri kufuata mwongozo wa kupunguza hatari ya unywaji pombe, kwa:

  • Kunywa vinywaji 2 pekee kwa siku kwa wanawake
  • Kunywa vinywaji 3 pekee kwa siku kwa wanaume

Kama ungependa kupunguza kunywa pombe, unaweza ukajaribu namna zifuatazo.

Fikiri kabla ya kunywa pombe

Je unahitaji kunywa au unakunywa kwa sababu ni tabia yako? Kama umezoea kunywa pombe wakati Fulani, jaribu kufanya kitu kingine wakati huo. Usiangalie sana matangazo ya pombe. Kadri unavyopunguza kuangalia matangazo ya pombe unapokuwa ukiangalia mpira au micheo mingine kwenye TV au mtandao ndivyo inakuwa rahisi Zaidi. Unaweza kufikiria pia kupigia upatu kupunguzwa kwa matangazo ya pombe katika jamii unayoishi.

Tafuta vitu mbadala

Tafuta vinywaji mbadala visivyo na pombe unavyoweza kufurahia, kwa mfano kunywa chai ya asali, tonic yenye kipande cha limao. Au kunywa bia isiyo na pombe.

Kunywa maji mengi Zaidi

Tumia maji kukata kiu yako. Kunywa glasi ya maji kaba haujaanza kunywa pombe. Kunywa maji Zaidi kwa kila kinywaji unachokunywa au katikati ya kila kinywaji.

Punguza kasi ya unywaji wako wa pombe

Hesabu vinywaji unavyokunywa. Ni rahisi kunywa haraka kama haufikirii. Kunywa taratibu ili kuhakikisha kinywaji kinachua muda mrefu kumalizika.

Piga hesabu

Jumlisha ili kujua umetumia shilingi ngapi kwa ujumla kila unapokunywa kila mwezi. Ni kiasi gani kwa mwaka mzima. Kama ukiunguza kiwango unachokunywa, unaweza kufanya nini na pesa hiyo?

Jipatie likizo ya pombe

Chagua siku 2 au Zaidi katika wiki ambazo haunywi pombe kabisa. Jaribu kujiangalia unajisikiaje katika siku hizi ambazo haunywi, kiakili, kimwili na kihisia. Uliweza kupata usingizi? Unajisikia vizuri? Kadri muda unavyokwennda, ongeza siku unazojipa likizo.

Hesabu kalori unazokunywa. Je, ungependa kupunguza uzito? Hili linaweza kuwa jambo bora sana linaloweza kukutia moyo kupunguza kunywa. Jaribu kupiga hesabu ni kiwango gani cha kalori unachoongeza mwilini kila unapokunywa kinywaji kimoja. Je kinaongeza kalori kiasi gani kwa siku? Kwa wiki? Kwa mwezi?

Sema hapana

Jifunze kusema hapana mtu anapokununulia kinywaji. Jaribu ‘’Asante sana ila mimi zimenitosha kwa leo’’ Au ‘’ asante sana, ila kwa sasa najaribu kupunguza kiwango nachokunywa’’ Au ‘’Asante sana, ila najisikia vizuri Zaidi nikinywa kidogo’’

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaii kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/patientinstructions/000857.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *