Maelezo ya jumla

Kwa kawaida nta masikioni hutengenezwa kwa kiwango kidogo tu ili kulinda sikio na kisha kutawanyika yenyewe. Lakini kama nta inayotengenezwa kwenye sikio ni nyingi sana, inaweza kujaa kwenye sikio, ikakakamaa baada ya kukauka na kuziba kabisa njia ya sikio. Ukitumia vijiti vya kusafisha ili kuondoa nta masikioni, vinaweza kuisukumia ndani na kuchangia kwa kiasi kikubwa kuziba kwa sikio. Nta ikijaa masikioni inaweza kusababisha mtu asisikie vizuri. Inaleta karaha na wakati mwingine inaweza kusababisha ujisikie masikio yamejaa. Masikio yanaweza kuwasha, ukapatwa na kizunguzungu au kusikia kelele masikioni.  Tatizo la kujaa kwa nta kwenye masikio linawapata zaidi wazee na watu wanaotumia vifaa maalumu ili kusikia hasa watu wenye matatizo ya kusikia

Mwone daktari kama una nta masikioni na;

Panga kuonana na daktari kama umegundua kuna nta masikioni, hasa kama umewahi kuwa na matatizo ya sikio hapo kabla.

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kama una nta masikioni

Unapaswa kutibu au kuondoa nta kwenye masikio pale tu unapoona kuwa zinakuletea matatizo. Unaweza kutumia njia zifuatavyo ili kuondoa kabisa nta iliyojaa kwenye sikio. Kama una miadi na daktari ya kuodoa nta kwa kutumia bomba la sindano, unawea pia kufuata hatua hizi ili kulainisha nta kabla haujaenda kumwona.nta masikioni

  • Epuka kutumia au kuingiza vijiti vya kutolea uchafu ‘’cotton swab’’ au kitu chochote kwenye sikio ili kuondoa nta.
    • Ukifanya hivi, unasokomeza nta ndani zaidi na kusababisha iwe ngumu kuzitoa.
    • Unaongeza uwezekano wa kuharibu sehemu ya ndani ya sikio, kusababisha usumbufu na hata maambukizi au unaweza kuharibu kabisa ngoma ya sikio
  • Tibu sikio na dawa/kitu ambacho kitalainisha nta masikioni. Jaribu kutumia mafuta ya mzeituni ‘’olive oil’’ au mafuta ya mlozi ‘’almond oil’’
    • Unaweza kutumia kidondosheo kinachokuwa kwenye chupa yenye mafuta ya kulainisha nta, mwombe mfamasia au mtu yeyote akudondoshee matone kadhaa kwenye sikio.
    • Kama masikio yote yameziba, subiri kwanza mpaka moja liwe limezibuka ndio uweke kwenye jingine la pili. Hii ni kwa sababu, nta inapoanza kulainika inatawanyika na inaweza kuziba zaidi sikio kwa muda. Ni vizuri kutibu sikio moja baada ya jingine ili angalau kubakiza uwezo wa kusikia.
    • Kabla hujatumia mafuta ya mzeituni au ya mlozi, yapashe kwanza kwa muda wa nusu saa mpaka saa nzima ili yapate joto au unaweza kuyaweka kwenye kibakuli chenye maji ya moto ili kuyapasha kabla ya kuyatumia (yasiwe ya moto sana yakakuunguza)
    • Ukiwa umelala na sikio liloathirika likiwa juu, tumia kidondosheo cha kwenye chupa na dondosha matone 3-4 ya mafuta kwenye njia ya sikio.
    • Subiri kwa dakika 10 ili mafuata yaingie vizuri na kunyonywa na nta na kisha futa mafuta yaliyobakia
    • Rudia mchakato huu mara 3 kwa siku, kwa siku 5
  • Kama mbadala, unaweza kutumia madawa maalumu yaliyotengenezwa ili kuyeyusha nta ‘’Earwax drops’’. Dawa hizi zinaweza kutumiwa ili kuyeyusha nta. Zina ”carbamide peroxide” ambayo wakati mwingine inaweza kusumbua sikio. Omba ushauri kwa mfamasia kwa ushauri zaidi

Mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

  • Kama bado unahisi siki limeziba hata baada ya kuumia njia hizi za kujisaidia bila mafanikio
  • Kama unaanza kusikia sikio linauma au unaona kuna uchafu au usaha unatoka kwenye sikio

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000979.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *