Maelezo ya jumla
Pumu ya ngozi (eczema), ni neno linalotumika kuwakilisha aina mbalimbali za uvimbe wa ngozi. Tatizo hili hujulikana pia kama ugonjwa wa ngozi (dermatitis). Pumu ya ngozi sio hatari na hauambukizwi, lakini aina nyingi husababisha ngozi kuwa nyekundu, kuvimba na kuwasha. Mambo ambayo yanaweza kusababisha shida hii ni pamoja na magonjwa, vitu vinavyowasha, mzio au aleji na muundo wa kijenetiki. Aina inayowapata watu wengi ni ”atopic dermatitis”. Hii ni hali ya mzio ambayo hufanya ngozi kuwa kavu na kuwasha. Inawatokea zaidi watoto wachanga na watoto wakubwa. Pumu ya ngozi haiwezi kuponywa kabisa, lakini mtu anaweza kuzuia aina fulani za tatizo hili kwa kuepuka kukutana na vitu vinavyowasha, msongo wa mawazo na vichochezi vya mzio.
Je,ni nini dalili za Pumu ya ngozi ?
Pumu hii si ugonjwa mmoja, kuna aina nyingi na kila aina huonesha mkusanyiko wa dalili nyingi tofauti. Kuvimba kwa ngozi ni dalili inayopatika katika aina zote. Zifuatazo ni dalili za aina kadhaa za Pumu ya ngoz
- Atopic Eczema -Hii ndio aina inayowapata watu wengi zaidi, inafikiriwa kuwa aina hii ina uhusiano wa kijenetiki na pumu. Mzio husababisha Pumu hii ya ngozi kutokea sehemu yoyote ya mwili hata kama sehemu hiyo haijagusana na kizio (Kizio -(allergen) ni kitu chochote kinachochochea kutokea kwa mzio). Vipele vinavyowashawa hutokea hasa kichwani, shingoni, sehemu ya ndani ya kiwiko, sehemu ya nyuma ya magoti na kwenye matako.
- Contact dermatitis- hii ni aina inayotokea baada ya kugusa kizio au kitu chochote kinachoweza kusababisha harara, kwa mfano mgonjwa anayetumia kemikali kusafishia nyumba anaweza kupata Pumu hii ya ngozi baadae, mikono yake inaweza kupata vipele na kuwasha na hata kuchubuka.
- Eczema Xerotic – Ngozi ya mgonjwa huwa kavu sana na kupasuka pasuka ,baadae hutengeneza vipele. Mara nyingi hali hii huwapata zaidi wazee
- Seborrhoeic dermatitis – Ngozi ya kichwa, kope, uso na kiwiliwili huanza kubanduka , ngozi ya sehemu hizi inaweza kuwa kavu au yenye mafutamafuta.
Uchaguzi wa matibabu ya Pumu ya ngozi
Hakuna tiba ya kukuponya kabisa tatizo hili, lakini kuna matibabu kadhaa yanayopunguza uvimbe na kuwasha:
- Corticosteroids:-dawa hizi zinatofautiana, kuna ambazo zina nguvu kuliko zingine, na daktari huzitoa kulingana na ukali wa ugonjwa wako. Dawa hizi zikitumiwa kwa muda mrefu zinaweza kuwa na madhara, kama vile; kusababisha ngozi kuwa nyembamba sana na kusababisha maambukizi kwenye ngozi. Dawa hizi hazipendekezwi kutumika kama kinga.
- Mafuta ya kukinga ngozi- mafuta haya yanayotengenezwa kwa ceramides, free fatty acids na lehemu hunuia kurekebisha ngozi iliyoharibika.
- Immunomodulators:-hupunguza mfumo wa kinga katika maeneo yaliyoathirika. Dawa hizi mara nyingi hutumiwa zaidi katika hali kali sana za ukurutu, hii ni kwa sababu zinafikiriwa kuwa zinaweza kuchangia kutokea kwa saratani ya tezi za limfu au ngozi.
- Antibiotiki – Kwa maambukizi yoyote yanayotokea baada ya ngozi kuharibiwa na ukurutu.
- Dawa za kupunguza kuwashwa
Magonjwa yenye dalili zinazofanana na Pumu ya ngozii
Kwa sababu shida hii wakati mwingine husababishwa na chakula, mara nyingi watu huchanganya mzio wa chakula na Pumu ya ngozi.
Kuzuia Pumu ya ngozi
- Watu wenye tatizo hili, au watu wanaoishi na mtu aliye na Pumu ya ngoz, ambao hawako katika hatari ya ya kupata ndui (smallpox), inashauriwa wasipewe chanjo ya ndui kwa sababu inaweza kusababisha vidonda vya chanjo.
- Ongeza unyevunyevu kwenye ngozi. Epuka kutumia sabuni na madawa makali.
- Hatua za kimazingira, kama vile kuepuka vumbi. .
- Mlo, Wagonjwa wanapaswa kuepuka aina ya chakula fulani kinachochochea kutokea kwa ukurutu.