Mfumo wa chakula

Safari ya chakula ni ndefu na muhimu.

Umeng’enyaji wa chakula huanza pindi tu chakula kinapongia mdomoni na kutafunwa.

Mdomoni chakula hutafunywa na kutengeneza tonge moja linaloweza kumezeka.

Wakati wa kumeza chakula, ulimi hunyanyuka juu na kulielekeza tonge linapotoka kinywani.

Tonge hupita kwenye koo na baada kuingia kwenye umio.

Misuli ya umio inayokaza na kuachia hulisukuma tonge mpaka kufika tumboni

Misuli ya tumbo huendelea kukaza na kuchia ili kuvunja vunja chakula na kukichanganya na kemikali za umeng’enyaji zilizomo.

Chakula kilichomeng’enywa tumboni huvuka na kuelekea kwenye utumbo mdogo.

Vimeng’enya vilivyo kwenye utumbo mdogo huendelea kumeng’enya chakula kadri kinavyoshuka chini.

Ni kiasi kidogo tu cha virutubisho hufyonzwa chakula kinapokuwa tumboni

kiasi kikubwa cha ufyonzwaji wa virutubisho hufanyika kwenye utumbo mdogo.

Kuta za utumbo mdogo zimejaa viungo maalumu vinavyofanya kazi ya kufyonza virutubisho na kuvipeleka kwenye damu.

Kuna kiasi kidogo cha virutubisho vinavyoendelea kufyonzwa chakula kinapofikia utumbo mpana.

Kadri chakula kilichobakia bila kumeng’enywa kinapoendelea kupita kwenye utumbo mpana, kinaendelea kuwa kigumu na kutoka kama kinyesi.

Ni muhimu kulinda safari ya chakula mwilini.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/digestivesystem.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *