Maelezo ya jumla

Kibofu (bladder) hupatikana kwenye sehemu ya chini ya tumbo, na kazi yake kubwa ni kuhifadhi mkojo. Saratani ya kibofu (bladder cancer) hutokea kwenye utando wa ndani wa kibofu.

Je, nini dalili za kansa ya kibofu?

Dalili za kansa ya kibofu ni pamoja na:

Je! nini husababisha saratani ya kibofu?

Mara nyingi saratani ya kibofu husababihwa na :

  • Tibakemikali ”chemotherapy” – Dawa ya ”cyclophosphamide” inaweza kuongeza hatari ya kutokea kwa saratani ya kibofu.
  • Tiba ya mionzi – Wanawake waliowahi kupata tiba ya mionzi ili kutibu saratani ya shingo ya kizazi , wako kwenye hatari ya kupata kansa ya kibofu.
  • Maambukizi kwenye kibofu – Maambukizi ya kibofu ya muda mrefu (sugu) yanaweza kusababisha aina fulani ya saratani ya kibofu mf; Maambukizi ya kichocho

Nani yuko kwenye hatari ya kupata saratani ya kibofu?saratani ya kibofu

Sababu zinazoongeza hatari ya kupata saratani ya kibofu ni pamoja na:

  • Umri – Uwezekano wa kupata saratani ya kibofu huongezeka kadri umri unavyoongezeka. Watu wenye umri chini ya miaka 40 hupata saratani hii mara chache sana.
  • Sigara – Kuvuta sigara huongeza sana hatari ya kupata kansa ya kibofu. Karibia nusu ya kesi za saratani ya kibofu zinazowapata wanaume na kadhaa kwa wanawake husababishwa na uvutaji wa sigara.
  • Kemikali – Moja kati ya kesi nne za saratani ya kibofu husababishwa na kukutana na kemikali zinazosababisha kansa. Watu wanaofanya kazi ya kupaka rangi, wanaofanya kazi kwenye viwanda vya mpira, alumini na ngozi na wanaotumia dawa kali za kuua wadudu.
  • Tibakemikali – Dawa za tibakemikali kama ”cyclophosphamide” zinaweza kuongeza hatari ya kansa ya kibofu.
  • Tiba ya mionzi – Wanawake waliowahi kupata tiba ya mionzi kutibu kansa ya shingo ya kizazi, huwa kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu.
  • Maambukizi ya kibofu – Maambukizi ya kibofu ya muda mrefu (sugu) yanaweza kusababisha aina fulani ya saratani ya kibofu.
  • Asili – Wazungu hupata saratani ya kibofu mara mbili zaidi ya watu weusi. Viwango vya chini zaidi ni miongoni mwa Waasia.
  • Kuwa mwanaume – Wanaume hupata saratani ya kibofu mara mbili mpaka mara tatu zaidi ya wanawake.
  • Historia ya familia – Watu wenye mtu kwenye familia mwenye saratani ya kibofu huwa katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.

Ukiwa na saratani ya kibofu ni wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone daktari mara moja kama unapata dalili yoyote inayohusishwa na saratani ya kibofu

Utambuzi wa saratani ya kibofu

Kama mgonjwa ana dalili zinazoonesha kuwa ana saratani ya kibofu, daktari anaweza kuagiza moja au zaidi ya yafuatayo kufanyika:

  • Uchunguzi wa mwili – Daktari atachunguza sehemu ya chini ya tumbo kuangalia kama kuna uvimbe. Uchunguzi huu wa mwili unaweza kujumuisha uchunguzi wa njia ya haja kubwa na uke.
  • Vipimo vya mkojo – Maabara huuchunguza mkojo ili kuangalia kama kuna damu, seli za kansa, na ishara nyingine za ugonjwa.
  • ”Intravenous pyelogram”Wakati wa kipimo hiki, Daktari huchoma mgonjwa sindano yenye rangi maalumu, kwenye mshipa wa damu. Rangi hiyo hujikusanya kwenye kibofu cha mkojo na kusababisha kibofu kuonekana vizuri sana kwenye picha ya eksirei.
  • ”Cystoscopy” Daktari hutumia ”tube’nyembamba yenye kamera, inayoingizwa kupitia kwenye ”urethra” ili kuchunguza kibofu. Mgonjwa anaweza kuhitaji sindano ya ganzi kabla utaratibu huu haujafanyika.

Uchaguzi wa matibabu ya saratani ya kibofu

Upasuaji

  • Upasuaji ni tiba inayotumika mara nyingi kutibu kansa ya kibofu. Aina ya upasuaji hutegemea hatua/stage ya uvimbe.
  • Aina za upasuaji zinazotumika kutibu kansa ya kibofu ni pamoja na:
    • ”Transurethral resection”: Aina hii ya upasuaji hufanyika katika hatua za mwanzo za saratani. Daktari huingiza cystoscope yenye kamera ndani ya kibofu kupitia kwenye urethra (mrija huu unaotoa mkojo nje kutoka kwenye kibofu kupitis tundu la mkojo) na kutumia kifaa kidogo cha umeme kukwangua kansa yote na kuchoma seli zote za kansa zilizobakia kwa umeme. Baada ya upasuaji mgonjwa anaweza kuhitaji tibakemikali pia.
    • ”Radical cystectomy”: Aina hii ya upasuaji hufanyika kutibu kansa ya kibofu iliyovamia na kuharibu kibofu kabisa. Daktari huondoa kabisa kibofu cha mkojo, tezi za limfu zilizo karibu, sehemu ya ”urethra” na viungo vilivyokaribu vinavyoweza kuwa na seli za kansa. Tezi dume na mirija ya kubeba shahawa inaweza kuondolewa kwa wanaume. Kwa wanawake, uterasi, ovari, mirija ya uzazi, na sehemu ya uke inaweza kuondolewa.
    • ”Segmental cystectomy”: Katika hali nyingine, daktari anaweza kuondoa sehemu tu ya kibofu. Daktari anaweza kuchagua aina hii ya upasuaji kama kansa imeenea katika sehemu ndogo ya kibofu.

Tiba ya mionzi

  • Tiba ya mionzi hutumia miali nunurishi(radioactive) kuua seli za saratani. Kama ilivyo kwenye upasuaji, tiba ya mionzi huathiri seli za eneo linalotibiwa pekee.
  • Idadi ndogo ya wagonjwa wanaweza kupata tiba ya mionzi kabla ya upasuaji ili kupunguza ukubwa wa uvimbe kabla ya upasuaji. Wengine wanaweza kupata tiba ya mionzi baada ya upasuaji ili kuua seli za saratani zilizobakia baada ya upasuaji. Wakati mwingine, wagonjwa ambao hawawezi kuhimili upasuaji hupata tiba ya mionzi pekee.
  • Aina za tiba ya mionzi ni:
    • Tiba ya mionzi ya nje (External radiation therapy) – hutumia mashine iliyowekwa nje ya mwili na kuelekeza mionzi kwenye eneo lenye saratani. Watu wengi wanaopokea mionzi ya nje hutibiwa siku 5 kwa wiki 5 hadi 7 kama wagonjwa wa nje.
    • Tiba ya mionzi ya ndani (Internal radiation therapy) – Daktari huweka chombo kidogo chenye dutu ya mionzi ndani ya kibofu kupitia kwenye urethra au kwa kufanya upasuaji mdogo kwenye sehemu ya chini ya tumbo. Mgonjwa hulazwa hospitalini kwa siku kadhaa wakati wa matibabu. Ili kuwalinda watu wengine kutokana na mionzi, wagonjwa wanaweza kutengwa kwa kitambo kidogo. Hakuna mionzi inayobakia mwilini mara baada ya dutu yenye mionzi kuondolewa mwilini.

Tibakemikali

  • Kwa wagonjwa wenye saratani ambayo haijavamia kibofu, daktari anaweza kuagiza intravesical chemotherapy baada ya kuondoa kansa kwa upasuaji. Daktari huingiza bomba (catheter) kupitia kwenye urethra na kuweka dawa ndani ya kibofu. Dawa hii hubakia ndani ya kibofu kwa saa kadhaa. Kwa kawaida, mgonjwa hupata tiba hii mara moja kwa wiki kwa wiki kadhaa. Wakati mwingine, matibabu yanaweza kuendelea mara moja au mara kadhaa kwa mwezi mpaka mwaka.
  • Ikiwa saratani imevamia kibofu au kuenea mpaka kwenye tezi za limfu na viungo vingine, daktari anaweza kutoa dawa kupitia kwenye mshipa. Dawa hizi hutolewa kwa mzunguko ili kuwepo kipindi cha kupumzika kati ya mzunguko mmoja wa tiba na mwingine.
  • Kwa kawaida tibakemikali hutolewa kwa wagonjwa wa nje, lakini kulingana na dawa zinazotolewa na afya ya mgonjwa kwa ujumla, mgonjwa anaweza kuhitajika kulazwa hospitalini kwa muda mfupi.

Kuzuia kansa ya kibofu

Hakuna kipimo au njia maalumu ya kuzuia saratani ya kibofu.

Nini cha kutarajia unapopata kansa ya kibofu?

Matarajio ya mgonjwa mwenye kansa ya kibofu hutegemea eneo na hatua ya ugonjwa. Inapogunduliwa mapema, kuna nafasi nzuri ya kupona kuliko inapagundulika katika hatua mwisho.

Matatizo yanayoweza kutokea ukiwa na kansa ya kibofu

  • Saratani ya kibofu inaweza kuenea mpaka kwenye viungo vingine. Inaweza pia kuenea mpaka kwenye tezi za limfu, ini, mapafu na mifupa.
  • Matatizo mengine yanayotokana na kansa ya kibofu ni pamoja na:
    • Anemia (upungufu wa damu)
    • Kupanuka kwa mirija inayotoa mkojo kwenye figo na kupeleka kwenye kibofu (hydronephrosis of ureters)
    • Kuziba kwa urethra (mrija wa kutoa mkojo kwenye kibofu kwenda nje)
    • Kushindwa kudhibiti mkojo/ kujikojolea

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/bladdercancer.html#cat11

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *