Saratani ya kizazi ni nini?

Saratani ya kizazi (endometrial cancer) ni saratani inayotokea kwenye utando wa ndani wa mji wa mimba (uterasi), na ni kansa nambari nne kwa kansa zinazowapata wanawake duniani.

Ni zipi dalili za saratani ya kizazi?

Dalili inayowapata wagonjwa wengi ni kutokwa na damu isivyokawaida ukeni. Kama umeshafikia ukomo wa hedhi (menopause), aina yoyote ya damu itakayotoka ukeni sio ya kawaida. Kama haujafikia ukomo wa hedhi bado, kama kiwango cha damu inayotoka kitaongezeka au kama unapata hedhi mara nyingi kuliko kawaida, au kama unatokwa damu katikati ya kipindi kimoja cha hedhi na kingine, hii sio kawaida. Ni vizuri kumwambia daktari kama unapata dalili hizi.

Kwa baadhi ya wanawake, saratani ya kizazi inaweza kusababisha kutokwa kwa majimaji mepesi, au uchafu mweupe mwepesi. Wanawake wengi wanaotokwa damu au kutokwa na uchafu hawana kansa. Kwa hiyo, mwone daktari ili atambue tatizo lako. Dalili nyingine ni pamoja na:

Hata hivyo, dalili hizi pia zinaweza kutokea kwa sababu ya matatizo mengine ya kiafya. Ni vizuri kumwona daktari ili afanye utambuzi.

Mambo yanayoongeza hatari ya kupata saratani ya kizazi?

Ukiwa na kiwango kikubwa cha homoni ya estrojeni kunaweza kukuweka katika hatari ya kupata saratani ya kizazi. Ongezeko la kiwango hiki cha homoni kinaweza kusababishwa na:

  • Kuwa na uzito mkubwa wa mwili / kitambi
  • Kama haujawahi kuzaa / kupata mtoto
  • Ugumba
  • Kuchelewa kwa damu ya hedhi kukata (kma unaendelea kupata damu ya hedhi baada ya 52 ya umri)
  • Kupata hedhi zisizotabirika
  • Kupata damu ya kwanza ya hedhi mapema sana (kupata damu ya kwanza kabla ya umri wa miaka 12) na,
  • Kutumia dawa zinazoongeza kiwango cha estrojeni mwilini (hasa kama zinatumiwa zenyewe bila kuunganishwa na homoni ya projesteroni)
  • Hatari pia inaongezeka abaada ya miaka 35 ya umri. Visa vingi vya saratani ya kizazi vinatokea kwa wanawake wenye umri wa mika 50 na 60.
  • Shinikizo la juu la damu
  • Ugonjwa wa kisukari, na
  • baadhi ya matatizo ya urithi, na kama kuna mtu katika familia mwenye au aliyewahi kupata saratani ya kizazi

Kuzuia saratani ya kizazi?

Hauwezi kuzuia saratani ya kizazi, lakini unaweza kupunguza hatari ya kuipata. Kutumia dawa za kupanga uzazi zenye vichocheo viwili (vidonge vya majira vyevye homoni ya estrojeni na projestroni) kunaweza kukulinda na saratani ya kizazi. Kudhibiti uzito wa mwili ni muhimu sana pia.

Je, ninapaswa kufanyiwa vipimo?

Kama hauna dalili zozote, hauhitaji kufanyiwa vipimo. Kama una dalili, daktari anaweza kupendekezwa upige picha ya mji wa mimba (ultrasound) au anaweza kuagiza ichukuliwe sampuli ya tishu ndogo kutoka kwenye mji wa mimba ili akaangaliwe kwa darubini kama kuna seli za kansa. Utaratibu huu unitwa biopsy kitaalamu. Kama hauwezi kufanyiwa utaratibu wa biopsy, daktari anaweza kuagiza ufanyiwe utaratibu mwingine wa kupanua mlango wa mji wa mimba na kukwangua utando wa ndani ya mji wa mimba (Dilatation and curettage). Utaratibu huu utamruhusu kuchukua sampuli kwa ajili ya kipimo. Usiwe na wasiwasi, utapewa dawa za kutosha kupunguza maumivu wakati utaratibu huu unapofanyika.

Saratani ya kizazi inatibiwaje?

Matibabu ya saratani ya kizazi yanategemea ugonjwa umesambaa kiasi gani. Matibabu yanayopendelewa sana ni kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mji wa mimba na ovari. Upasuaji huu unaondoa kabisa kizazi cha mwanamke.

Aina nyingine za matibabau ni pamoja na:

  • Tiba mionzi ili kudumaza/ kuua seli za saratani
  • Tiba ya kutumia homoni ili kupunguza kasi ya ukuaji wa kansa
  • Tiba kemikali ili kuua seli za saratani

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/imagepages/9294.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *