Tatizo la Shahawa zilizochanganyika na damu ni nini?
Shahawa zilizochanganyika na damu ni tatizo la kuwa na shahawa zilizochanganyikana na damu. Tatizo hili linawapata zaidi vijana wenye umri chini ya miaka 4o, lakini wanaume wa umri wowote wanaweza pia kulipata. Sababu za tatizo hili kwa vijana chini ya umri wa mika 40, huwa sio hatari sana.
Nitajuaje kama ni tatizo la Shahawa zilizochanganyika na damu?
Kama ukiona Shahawa zilizochanganyika na damu baada ya kushiriki tendo la ngono, zinaweza kuwa zinatoka kwako au kwa mwenzi wako. Ni vizuri kumuuliza mwenzi wako kama anakaribia kupata damu ya hedhi. Ni vizuri pia kuuliza kama mwenzi wako ameshawahi kupata ugonjwa wa ngono.
Nini kinaweza kusababisha tatizo la Shahawa zilizochanganyika na damu?
Mara nyingi, hakuna sababu maalumu inayofahamika. Linaweza kusababishwa na kukaa kipindi kirefu bila kushiriki ngono, kupiga punyeto/kujichua sana, au kushiriki ngono kwa muda mrefu sana. Sababu nyingine zinaweza kutegemea umri.
Unaweza kuhitaji kumwona daktari kama una umri wa miaka 40 na zaidi, kama una dalili nyingine, au kama hali hii itatokea zaidi ya mara 10 kwa mfululizao. Ni vizuri kuonana na daktarin haraka iwezekanavyo kama una homa, kutetemeka, au unatokwa jasho usiku, au kama unajihisi kuugua.
Sababu za kawaida zinazoweza kusababisha tatizo la Shahawa zilizochanganyika na damu ni:
- Maambukizi (hii ni pamoja na maambukzi ya magonjwa ya ngono)
- Uvimbe kwenye kibofu, tezi dume, au maeneo mengine yanayohusiana na haya
- Jeraha kwenye via vya uzazi
Kwa wanaume wenye umri zaidi ya miaka 40, sababu za nyongeza ni pamoja na:
- Taratibu za kimatibabu zinazohusisha via vya uzazi (kwa mfano kuchukua kinyama kwenye tezi dume (biopsy) kwa ajili ya kipimo au matibabu ya bawasiri)
- Matatizo ya kimuundo ya via vya uzazi, tezi dume, au mrija wa njia ya mkojo
- Saratani (hii ni pamoja na saratani ya tezi dume)
- Matatizo ya mishipa ya damu
Nitegemee nini nikienda kumwona daktari nikiwa na tatizo la Shahawa zilizochanganyika na damu?
Daktari atakuuliza kuhusu dalili ulizonazo, historia na mwenendo wa ngono, na kuhusu tabia hatarishi ulizonazo. Daktari anaweza kuhitaji kufanyia uchunguzi sehemu zako za siri na tezi dume.
Anaweza pia kuamua kufanya vipimo vya damu na vya mkojo. Kama ukiendelea kuwa na Shahawa zilizochanganyika na damu, daktari anaweza kukupa rufaa ili upate vipimo zaidi.
Tatizo la Shahawa zilizochanganyika na damu linatibiwaje?
Matibabu yanategemea sana sababu. Kwa kawaida, tatizo la Shahawa zilizochanganyika na damu linakoma bila matibabu yoyote. Kama una maambukizi, unaweza kuhitaji dawa za antibiotiki. Kama hali ya kuwa na Shahawa zilizochanganyika na damu imetokana na sababu ambayo ni mbaya zaidi unaweza kuhitaji kutibiwa na dakatari bingwa wa mfumo wa mkojo – urologist.
Angalizo
Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaii kuhusu shida hii.