Shinikizo la juu la damu ni nini?

Presha wakati wa ujauzito – Kuongezeka kwa shinikizo la damu (pia huitwa shinikizo la juu la damu au presha) hutokea damu inapopita kwenye mishipa ya damu kwa shinikizo (presha) kubwa kuliko kawaida. Kuwa na shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito/ presha wakati wa ujauzito ni tatizo hatari sana. Kuna majina kadhaa yanayotumika kulingana na lini  na vipi mwili unaathirika

JINA INAANZA LINI MATATIZO MENGINE
PRESHA SUGU Shinikizo la damu linaloanza kuongezeka kabla ya ujauzito au kabla ya wiki ya 20 (miezi 41/2) ya ujauzito Kunaweza kuwepo au kusiwepo protini kwenye mkojo
PRESHA WAKATI WA UJAUZITO Shinikizo la damu linalooanza kuongezeka baada ya wiki 20 za ujauzito Hakuna protini kwenye mkojo

 

KIFAFA CHA MIMBA Shinikizo la damu linaloanza kuongezeka baada ya wiki ya 20 ya ujauzito Kuna protini kwenye mkojo

 

shinikizo kubwa la damu

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata presha wakati wa ujauzito?

Uko kwenye hatari zaidi ya kupata matatizo haya kama ulikuwa na presha kabla ya ujauzito au kama ulipata presha katika ujauzito uliopita au uliotangulia. Sababu nyingine zinazoongeza hatari ni pamoja na:

Je, presha wakati wa ujauzito inaweza kuzuiwa?

Kama ulipata viashiria vya kifafa cha mimba au kifafa cha mimba kabla ya wiki ya 34 ya ujauzito uliotangulia au kwa wakati wowote kwa mimba mbili au zaidi zilizotangulia, daktari anaweza kupendekeza utumie dawa ya aspirin kuanzia mwanzo wa ujauzito.

Baadhi ya madaktari wanapendekeza kutumia dawa ya aspirin kama una mapacha au kama una presha sugu, ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa figo, au ugonjwa wa lupus. Vidonge vya calcium vinaweza kusaidia kupunguza uwezekanao wa kupata kifafa cha mimba kama hauna kalisiamu ya kutosha kwenye mlo wako, lakini tatizo hili si kubwa Tanzania.

Nitajuaje kama nina presha wakati wa ujauzito?

Unaweza ukawa na dalili, lakini mara nyingi ni ngumu kujua. Moja ya sababu za kumwona daktari mara kwa mara ukiwa mjamzito ni hii. Pima kiwango cha shinikizo la damu mara kwa mara ukiwa mjamzito. Shinikizo lako la damu liko juu kama linazidi 140/90mmHg. Wanawake wengine wenye presha wanapatwa na maumivu ya kichwa, kushindwa kuona vizuri, maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo, au kuvimba mikono na uso. Ni vizuri kumwona daktari haraka kama unaona dalili hizi, hasa baada ya miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito kupita.

preshaPresha ya ujauzito inatibiwaje?

Unaweza kuhitajika kutumia dawa au kubakia hospitali kupata matibabu kwa muda fulani. Inategemea ujauzito una umri gani, wakati mwingine daktari atahitajika kuanzisha uchungu ili ujifungue mapema kuliko ilivyotarajiwa. Kama dakatari ataamuaku anzisha uchungu ili ujifungue kabla ya wiki 34 za ujauzito, utahitaji kuchomwa sindano za steroid ili kusaidia mapafu ya mtoto kukua haraka tayari kwa kazi ya kupumua atakapotoka.

Je, Presha ya ujauzito itaondoka baada ya kujifungua?

Mara nyingi, tatizo la presha wakati wa ujauzto linaanza kuondoka mara tu baada ya kujifungua. Lakini unapaswa kujua kuwa, kuna baadhi ya wananwake wanaweza kuanza kupata presha ya ujauzito au viashiria vya kifafa cha mimba mara baada tu ya kujifungua mtoto, na hali inaweza kuwa mbaya sana kabla haijaanza kuboreka.

Ni vizuri kuonana na daktari mapema iwezekanavyo kama una maumivu ya kichwa, kushindwa kuona vizuri, maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo, au kama unavimba sana mikono baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.

Inaweza kuchukua mpaka wiki 12 baada ya mtoto kuzaliwa kwa presha ya mwili kurudi kuwa kawaida. Kama haitorudi kuwa kawaida, inamaanisha una ugonjwa wa presha sugu na utahitajika kuendelea kutumia dawa za kudhibiti presha maisha yako yote au kama daktari anavyoelekeza.

Kama una viashiria vya kifafa cha mimba, kuna uwezekano mkubwa kuwa utapata presha sugu hapo baadae, uko kwenye hatari pia ya kuwa na ugonjwa wa kisukari, na magonjwa ya moyo katika kipindi cha maisha yako. Ni vizuri kuongea na daktari ni kwa mara ngapi utahitaji kufanya vipimo. Badili mfumo wako wa Maisha pia.

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://www.nhlbi.nih.gov/health/high-blood-pressure/pregnancy

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *