Maeleo ya jumla
Kama unatatizo la kusikia kelele masikioni au kichwani (tinnitus), unahisi kama kengele inapigiwa masikioni, sauti ”buzzz” kama mdudu anayeruka au sauti ”hissss” kama nyoka. Unasikia sauti kama zinaanzia masikioni au kichwani na ukitafuta chanzo cha kelele hizi kwenye mazingira uliyopo hakipo. Kelele hizi zinaweza kuwepo muda wote au zinaweza kuwa zinakuja na kuondoka. Zinaweza kusababisha ukashindwa kupata usingizi, ukashindwa kufanya vitu kwa umakini, na ukapatwa na ugonjwa wa sonona.
Kadri muda unavyokwenda ukiwa na tatizo la kusikia kelele masikioni, unaweza kuanza kuwa mtu wa wasiwasi mwingi. Watu wanaopatwa na tatizo hili, mara nyingi hupoteza uwezo wa kusikia wanapofika uzeeni. Wengi wa waathirika huwa na historia ya kufanya kazi au kuishi maeneo yenye kelele nyingi. Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuchangia mtu kupata tatizo la kelele masikioni ni pamoja na:
- kusafiri kwa ndege
- Ongezeko la shinikizo la damu
- kujaa kwa nta kwenye masikio
- Matatizo kadhaa ya sehemu ya ndani ya sikio ‘’inner ear’’ na
- Baadhi ya madawa
Mwone daktari kama
Panga kumwona daktari ili atambue kama kusikia kelele masikioni au kelele unazosikia kichwani ni tatizo, na kama madawa unayotumia, kama vile ”Aspirin” yanachangia tatizo kuwa kubwa zaidi. Ni vizuri kumwona daktari ili atambue tatizo na kukupatia mpango wa matibabu
Mambo unayoweza kufanya wewe mwenyenwe kama unasikia kelele masikioni au kichwani
Sio watu wote wenye tatizo la kusikia kelele masioni watapata tiba ya kuponyesha kabisa tatizo hili, kuna baadhi ya wagonjwa tatizo hili kwao halina tiba ambayo inaweza kuliondoa kabisa. Lakini kuna baadhi ya mambo ukiyafanya yanaweza kupunguza madhara na karaha unayoisikia na kuboresha maisha yako
- Unaweza kujaribu kutumia sauti nyingine ili kuzifunika au kukuondoa kwenye kelele za masikio yako. Kama unajaribu kulala unaweza kuwasha feni ‘’fan’’, ukawasha mziki laini, ukasikiliza mlio wa saa inapopiga au unaweza kuwasha radio ili usikilize ile kelele ya ‘’hiss’’ wakati radio haishiki. Hii inaweza kukusaidia kupata usingizi.
- Linda masikio kwa kuweka vifunika masikio ‘’earplugs’’ wakati unapokuwa maeneo yenye kelele, au wakati unapotumia vifaa vya kazi vinavyosababisha kelele. Kwa mfano ‘’drill’’, kwa sababu kelele zinaweza kusababisha tatizo likawa baya zaidi.
- Punguza kunywa vinywaji vyenye ‘’caffeine’’ kama vile kahawa au cola. Epuka kunywa pombe, au kuvuta sigara. Vitu vyote hivi vinasababisha tatizo la kelele masikioni kuwa kubwa zaidi
- Kula mlo wenye chumvi kidogo inaweza kusaidia. Weka chumvi kidogo unapokuwa unapika, tumia viungo vingine kuongeza ladha ya chakula
- Kama msongo unasababisha tatizo hili la kelele masikioni kuwa kubwa zaidi, fanya mazoezi mara kwa mara na tafuta njia za kupunguza msongo kwenye maisha yako. BONYEZA HAPA KUJIFUNZA NJIA ZA KUPUNGUZA MSONGO
- Kama una tatizo la kusikia kelele masikioni ambalo halikomi na hakuna njia ya kuliondoa, tafuta watu wenye shida kama yako na uzungumze nao, itakuwa njia nzuri ya kuleta matatizo kwao na kutafuta suluhisho.
Tafuta matibabu kama unasikia kelele masikioni au kichwani
Panga kumwona daktari:
- Kama tatizo la kusikia kelele masikioni linazidi kuwa kubwa au kama haliitikii matibabu yaliyotolewa na daktari au kama njia za kujisaidia mwenyewe nilizozitaja hapo juu hazikusaidiii
- Kama unahisi kizunguzungu au kuhisi kuumwa
- Kama unaanza kupoteza uwezo wa kusikia
Je kuna daww zozote home made ambazo zinaweza kuondoa tinnitus.?
Je nitumie namna gani bizzari(turmeric) ili kuondoa tatizo hili
Onana na daktari tafadhali
Nikifanya mazoezi kelele zinakuwa kubwa zaidi..
ni vizuri kumwona daktari kama shida inaongezeka