Maelezo ya jumla

Watoto wengi na vijana ambao wako kwenye balehe wanauma au kutafuna kucha. Lakini wengi wao, kadri wanavyokua wanaiacha tabia hii. Baadhi ya watu, huendelea na tabia hii ya kula au kutafuna kucha mpaka utu uzima. Inaweza kuwa ngumu kweli kuacha tabia hii. Unaweza kujikuta ukitafuna kucha bila kujitambua, hasa unapokuwa hauna kazi au kama njia ya kujihami wakati ambao una msongo au sonona.
Japo tabia hii inakera, shida kubwa zaidi ni kuwa inasababisha iwe rahisi kuingiza uchafu au vimelea mdomoni. Kama una tatizo la kutafuna kucha na ngozi inayoizunguka, unaongeza uwezekano wa eneo hilo kupata maambukizi. Unaweza kuona aibu kucha zako kuonekana hasa kama hazina mwonekano unaopendeza.

Mwone daktari kama

Ni vizuri kupanga kumwona daktari kama:

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe nyumbanikutafuna kucha

Kama wewe au mwanao ameamua kuacha kula/kutafuna/kuuma kucha, unaweza kufuata hatua zifuatazo ili kuondokona na hili tatizo.

  • Kaa mbele ya kioo na kisha jiangalie unapokuwa unakula/kutafuna kucha, uone jinsi unavyoonekana.
  • Kata kucha ili ziwe fupi, na kisha zisawazishe vizurii ili kusiwe na ncha mbazo zitakushawishi kuzitafuna. Funga bandage kwenye ncha za vidole ili isiwe rahisi kuzifikia unapotaka kuzitafuna
  • Jaribu kujishtua unapotaka kuanza kutafuna kucha na jaribu kuipatia kazi mikono, chezea kalamu au nunua kimpira kidogo ili kukifinya unapohisi hamu ya kula kucha.
  • Tafuta ”gum” ambazo hazina sukari utafune badala ya kutafuna kucha
  • Unaweza pia kutumia ”antinail-biting lotion”, hii ni lotion yenye ladha chungu inayopakwa kwenye kucha. uchungu wa lotion hii unakukumbusha kuwa hupasw kuafuna kucha zako. unaweza kutumia lotion hizi kwa watoto wenye miaka zaidi ya 5 baada ya kukubaliana nae, usimlazimishe.
    • Wakati wa kutumia lotion hii, ipake kama unavyopaka rangi ya kucha mara moja kwa siku, kuwa makini usisahau sehemu ya juu au ncha ya ukucha
  • Jipongeze unapoanza kuona kucha zinaanza kupendeza na tabia inaanza kupungua
  • Unaweza kuamua kuweka au kupachika kucha za bandia. Kwa sababu kucha za bandia zinaweza kubaki kwa muda wa wiki 2, muda huu unaweza kutosha kabisa kupunguza tabia hii kama hautazitafuna.
  • Usifanye mwanao ajisikie mwenye hatia kwa sababu ya tabia ya kutafuna kucha. Tambua kuwa hata yeye anaichukia na hapendi kuendelea na tabia hiyo, sema tu anashindwa kuacha. Jaribu kutafuta kama kuna jambo linamsababishia msongo wa mawazo au linamtia wasiwasi mkubwa na kama unaweza kumsaidia
  • Unaweza kutumia chati ya nyota, wewe na mwanao. Kial siku ambayo ataweza kukaa bila kutafuna kucha unapatia nyota moja na mnunulie zawadi ndogo kila wakati chati yenu inapojaa nyota. Hii itamfanya ajitahidi kuacha tabia hii

Tafuta msaada wa daktari kama

Ni vizuri kupanga kumwona daktari kama:

  • Utakuta ngozi inayouzunguka ukucha imekuwa nyekundu au kama inatoa majimaji au kama inavuja damu baada ya kutafuna kucha

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003247.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *