Mtoto kuchelewa kuongea maana yake nini?

Kuchelewa kuongea kunaweza kusababisha mtoto kuwa na shida kutamka baadhi ya maneno na sentensi, anaweza kupata shida kuelewa kilichosemwa, au kushindwa kueleza hisia, mawazo na fikra zake kwa maneno.

Kila mtoto anakua kwa kasi yake mwenyewe, lakini kama mtoto atashindwa kuongea sawa na Watoto wengine wenye umri sawa na yeye, kunaweza kuwepo na tatizo la kuchelewa kuongea. Daktari anaweza kuhisi kuwa mtoto ana tatizo la kuchelewa kuongea kama:

  • Anashindwa kutamka angalau maneno matatu baada ya umri wa miezi 15
  • Anashindwa kufuatilia maelekezo ya hatua moja baada ya miezi 18
  • Anashindwa kuelekeza picha au sehemu za viungo kwenye picha mtu anapovitaja baada ya miaka miwili
  • Anashindwa kufuatilia maelekezo ya hatua mbili baada ya miaka mitatu ya umri

Ni nini husababisha tatizo la kuchelewa kuongea?

Matatizo ya kawaida yanayosababisha kuchelewa kwa mtoto kuongea ni pamoja na ukuaji duni, ukiziwi, au matatizo ya akili. Sababu nyingini ni pamoja na:

  • Mtindio wa ubongo
  • Tatizo la apraxia – tatizo linalosababisja iwe ngumu kuunda sauti kwa usahihi
  • Tatizo la dysathria – tatizo la kushindwa kuongea linalotokana na matatizo kwenye misuli inayotumika kutengeneza sauti na kuongea
  • Kuamua tu kutokuongea katika nyakati fulani – selective mutisim
  • Usonji

Je, Kuchelewa kuongea kunaweza kumpata mtoto kama mnazungumza lugha mbili nyumbani?

Mwanao anaweza kuchanganya lugha hizo mbili anapoanza kujifunza, lakini hii ni kawaida. Kufikia umri wa miaka mitano, mtoto wako atakuwa anaongea vyema kabisa lugha zote mbili.

Daktari atajuaje kuwa mtoto kachelewa kuongea?

Daktari atachunguza namna mtoto anavyoongea, uwezo wa akili na ukuaji wa mwili. Anaweza pia kuchunguza uwezo wa kusikia na kama kuna tatizo.

Kufanyike nini kama mtoto ana tatizo la kuchelewa kuongea?

Mtoto anaweza asihitaji matibabu yoyote. Baadhi ya Watoto wanahitaji muda mrefu zaidi ili kuanza kuongea. Daktari anaweza kukupatia rufaa ya kuonana na mtaalamu wa sauti ili amsaidie kuelewa na namna ya kutamka maneno. Mtaalamu wa lugha na sauti anaweza pia kukufundisha njia mbalimbali za kumsaidia mtoto na kumtia moyo ili aongee.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/speechandlanguageproblemsinchildren.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *