Maelezo ya jumla
Tatizo la sauti kukwaruza au kupotea ni shida inayokera, sauti yako inakua inakwaruza kwaruza na inakuwa ngumu wewe kusikika unapoongea. Sababu ya kawaida huwa ni kuvimba kwa sanduku la kutengenezea sauti ‘’voice box’’ kwa sababu ya maambukizi kama vile mafua. Koo linaweza kuwa linawasha au kuuma na unaweza kuwa unahisi kama kuna uvimbe kooni. Unaweza kupoteza sauti ghafla kwa sababu ya matumizi mabaya ya sauti – kwa mfano kama unaongea kwa nguvu sana au unashangilia kwa nguvu sana wakati wa mechi ya mpira wa miguu. Ukiona tatizo la kukwaruza kwaruza sauti linaanza taratibu linaweza kuwa limesababishwa na matumizi mabaya ya sauti, kuvuta sigara au kucheua kwa asidi ya tumbo ambayo pia inasababisha kiungulia na kusumbua sanduku la kutengenezea sauti kooni. Kwa kesi chache tu, kukwaruza kwaruza kwa sauti kunaweza kuwa dalili ya mwanzo ya kansa ya koo.
Unachoweza kufanya mwenyewe ukiwa na tatizo la sauti kukwaruza au kupotea
Kwa kawaida tatizo la kukwaruza au kupotea kwa sauti huwa ni la muda na huwa halidumu zaidi ya wiki moja. Ukifuata njia zifuatazo itasaidia kurudi haraka kwa sauti yako
- Pumzisha sauti kadri inavyowezekana. Usiongee au kunong’oneza. Kunong’oneza kunaweza kusababisha misuli ya koo kukaza zaidi kuliko hatanukiongea kawaida.
- Kunywa maji ya kutosha ili kupooza koo, kunywa angalau glass 6-8 za maji ili kuepuka koo kukauka sana. Usinye vinywaji vyenye caffeine kama vile kahawa, cola, chai au pombe
- Kula vyakula laini ambavyo vitakuwa rahisi kumeza
- Epuka kukaa maeneo yaliyo makavu sana au yenye moshi mwingi ambao unaweza kukausha zaidi koo na kusababisha hali ya sauti kuwa mbaya zaidi
- Kama koo linauma sana, tumia dawa za kupunguza maumivu, madawa kama vile ‘’acetaminophen’’ yatasaidia kupunguza maumivu ya koo na kukwaruza kwaruza kwa sauti
- Unaweza pia kujifukiza ili kupunguza kuvimba kwa koo na kuongeza unyevu kooni. Weka maji ya moto kwenye bakuli na kisha chukua kitambaa jifunike kichwani ukiwa umeinamia maji hayo ya moto (yasiwe yanachemka yakakuunguza). Vuta pumzi kupitia pumzi zako ili kuruhusu mvuke uingie
- Usi-gogomoe ‘’gargling’’ – haisaidii, madawa ya kikohozi pia hayasaidii kurudi kwa sauti pia
Kugogomoa
Mwone daktari kama
Kama una tatizo la sauti kuwaruza au kupotea panga kumwona daktari kama:
- Kama sauti yako bado inakwaruza kwa zaidi ya wiki 2 hata baada ya kufuata ushauri ulio hapo juu
- Kama sauti yako inakwaruza au imesha na unapata shida ya kupumua au unapata shida kumeza
Kuzuia tatizo la sauti kukwaruza au kupotea
Unaweza kulinda koo lako kama unapata tatizo la sauti kukwaruza au kupotea mara kwa mara. Jaribu kufanya mambo yafuatayo ili kupunguza uwezekano wa kujirudia
- Kunywa mai angalau glass 6-8 za maji kwa siku. Weka chupa ya maji karibu yako ukiwa kazini au nyumbani, piga pafu ndogo ndogo kila wakati
- Kama kazi yako inahusiana na kuongea na watu darasani au kwenye kikundi, jitahidi usiongee kwa nguvu au kukaza sana sauti. Panga makundi madogo madogo na kaeni akibu. Kama unapanga kuongea na kundi kubwa omba kipaza sauti
- Kupayuka au kuongea kwa nguvu kunaongeza mkazo mkubwa kwenye misuli ya kooni, jaribu kudhibiti hasira au wasiwasi wako kama unakufanya utumie vibaya sauti yako
- Acha kuvuta sigara na epuka kukaa kwenye mazingira yenye moshi mwingi
- Jitahidi usikohoe au kusafisha koo lako kwa nguvu
- Jaribu kuvuta pumzi kupitia kwenye pua zako. Ukivuta hewa ya baridi na kavu kupitia kwenye mdomo unasababisha mdomo na koo kukauka na kusababisha tatizo liwepo
- Kama unaishi eneo lenye baridi sana na unahitaji kupasha chumba chako tumia ‘’humidifier’’ au chukua bakuli la maji liweke karibu na ‘’radiator’’ ili kuongea unyevu chumbani
Thanks dr KWA elimu… Wikielimu n fire 💪
Asante sana Dr. , karibu tuuelimishe umma
Nashkr sana doctar kwani leo nimeenda kucheki ivo ila mimi niko petrol station vipi tatizo hilo linauhusiana san km ni sabbu moja wapo?
Ndio, kuvuta hewa ya mafupa ya petrol kwa muda mrefu sana inaweza kuleta tatizo hili, kama unafanya kazi katika kituo ch mafuta na eneo hilo halina mzungko mzuri wa hewa, kuvuta mafuta kwa muda mrefu kunaweza kukusababishia maumivu ya kichwa ya mara kwa mara, kizunguzungu na ikizidi sana hata kupoteza fahamu. Mvuke wa mafuta unaweza pia kusababisha koo kukauka, maumivu ya koo na hata kupotea kwa sauti na kama mvuke utaingia ndani kabisa ya mapafu unawea kukusababishia nyumonia/ kuvimba kwa mapafu ambako kunaweza kuwa hatari
mzunguko mzuri wa hewa ni muhimu katika eneo lako la kazi
Mbn nimetumia daw mpaka za maji lkn bdo saut aijakaa kama mwazo na kifua akiban wala koo kukwaruza
Kama unaona inakukera ni vzr kumwona daktari akifanyie uchunguzi na kukusaidia
Asante sana doctor, kwani nimekuwa na shida hii kwa muda sasa kuna muda mpaka niteme makoozi ndo napata ahueni kidogo ya koo na sauti, je asali na tangawizi inafaa kutumia doctor
Zinafaa