Tatizo/ugonjwa wa kujiona mbaya ni nini?
Ugonjwa wa kujiona mbaya ni hali inayokutokea unaposhindwa kujizuia kufikiria kuhusu sehemu fulani ya mwili. Unajihisi kama kuna shida fulani na sehemu fulani ya mwili, hata kama haina shida yoyote.
Tatizo/ugonjwa wa kujiona mbaya una dalili gani?
Unajikuta unaifikiria sana na kuwa na wasiwasi kuhusu sehemu fulani ya mwili. Muda mwingi unajihisi mwenye huzuni au kukata tamaa. Utajikuta unatamani kuficha au unaficha sehemu hiyo ya mwili unayoiwazia isionwe na watu wengine. Baadhi ya watu wenye ugonjwa wa kujiona mbaya wanaweza kuepuka kukutana na watu kabisa, kwa sababu hawataki watu waone sehemu hiyo wanayoiwazia kuwa ni mbaya. Hali hii inaweza kusababisha matatizo kazini au shuleni, na kwenye mahusiano.
Watu wenye Tatizo/ugonjwa wa kujiona mbaya wanawazia nini zaidi?
Baadhi ya watu wenye ugonjwa wa kujiona wabaya wanawazia zaidi sehemu za uso, lakini wengine wanawazia sehemu nyingine ya mwili. Mfano wa sehemu wanazoziwazia ni pamoja na:
- Kuwa alama au doa kwenye ngozi ni kubwa sana
- Chunusi zangu ni nyingi au mbaya sana
- Kovu ni kubwa mno
- Pua ni kubwa sana
- Meno yangu hayajanyooka, hayalingani
- Nina nywele nyingi sana usoni au mwilini
- Nina nywele kidogo sana kichwani
- Ukubwa na mwonekano wa matiti hauko sawa
- Misuli yangu ni midogo sana
Tabia gani zinaoneshwa na watu wenye Tatizo/ugonjwa wa kujiona mbaya?
- Kila wakati wanajiangalia kwenye kioo au kwenye vitu vinavyoweza kuakisi sura zao ili kuiangalia sehemu hiyo wanayoiwazia
- Kukwepa kujiangalia/ kukwepa kabisa kuwa karibu na kioo
- Wanaepuka au kukataa kupiga picha yoyote
- Kila wakati wanajiremba (kwa mfano. Wanabonyeza bonyeza chunusi, wananyoa kila wakati, kuchana nywele kila wakati)
- Kudonoa donoa au kushikashika ngozi ili kuiweka sawa
- Kuchunguza, kushika au kupima sehemu anayoiwazia mara kwa mara / mara nyingi
- Anajaribu kuificha sehemu anayodhani ina shida kwa kuvaa kofia, miwani au kupaka makeup nyingi
- Anakwenda kwa daktari, daktari bingwa wa upasuaji wa urembo, au daktari bingwa wa meno kila mara ili kurekebisha sehemu anayodhani ina shida
- Anafanyiwa taratibu nyingi, ikiwemo upasuaji kwa kitu kidogo au shida ndogo
Tatizo/ugonjwa wa kujionaa mbaya unatibiwa vipi?
Mwambie daktari kama una mawazo haya au dalili yoyote kati ya hizi. Daktari anaweza kukupatia dawa zinazoweza kusaidia. Daktari anaweza pia kukusaidia kukutafutia mtu wa kuongea nae (mtaalamu wa tiba maongezi – therapist) ambaye ana uzoefu kutibu ugonjwa huu. Mtaalamu anaweza kutumia njia inayofahamika kama cognitive behavior therapy ili kukusaidia. Hii ni aina ya tiba ya maongezi inayosaidia watu kufikiria kuhusu matatizo yao na kuyafikiria kwa mtazamo mwingine.