Mifupa

Mifupa yote 206 iliyoko kwenye mwili wa binadamu, hufanya kazi ya kuutegemeza, kuulinda na kuruhusu mwili kujongea.

Mifupa inalinda viungo muhimu vya mwili.

Ubongo umezungukwa na mifupa inayotengeneza fuvu.

Moyo na mapafu yamezungukwa na kulindwa na mifupa ya mbavu,

na mifupa ya  uti wa mgongo huutegemeza na kuulinda uti wa mgongo.

Mifupa pia, hufanya kazi ya kuhifadhi calcium na phosphorus na kutengeneza seli za damu.

Ushirikiano kati ya mifupa, misuli na mishipa ya fahamu husababisha mwili kufanya kazi yake.

Mifupa ni muhimu na inapaswa kulindwa.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/bonesjointsandmuscles.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *