Misuli

Tunahitaji misuli ili kuwa hai.

Karibia nusu ya uzito wa mwili wa mwanadamu unatokana na karibia misuli 600 inayofanya kazi ya kujongesha viungo mbalimbali.

Tishu za misuli zilizotapakaa mwili mzima, hukaza na kulegea ili kusaidia mwili kufanya kazi kikamilifu.

Tunahitaji misuli ikaze na kulegea ili tuendelee kuishi.

Misuli inalegea au kukaza kwa kuitikia ujumbe unaotumwa na mfumo wa fahamu.

Misuli laini inayopatikana katika viungo mbalimbali, hufanya kazi kwa kuitikia vichocheo vya homoni na jumbe zinazotumwa na mfumo wa fahamu.

Misuli inakaza na kusinyaa ili kufungia na kusukuma vitu katika mwili.

Mapigo ya moyo yanatokana na kukaza kwa misuli ya moyo inaposukuma damu.

Misuli ya moyo inafanya kazi bila kuchoka kwa kuitikia jumbe zinazotumwa na mfumo wa umeme unaopatikana kwenye moyo.

Tunahitaji kutunza misuli yetu ili kuwa hai.

  • Fanya mazoezi angalau dakika 150 kwa wiki,
  • Kula mlo kamili; mbogamboga, matunda, nafaka n.k.,
  • Kula vya kula vya protini kwa wingi: nyama isiyo na mafuta mengi, mayai, maharage n.k.,
  • Mwone daktari unapohisi kuugua.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/muscledisorders.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *