Maelezo ya jumla
Uchafu unatoka ukeni – ni hali ya kawaida kwa mwanamke kutokwa na uteute ukeni. Uteute huu huwa hauna rangi au unakua mweupe, kiasi na uzito wa uteute huu hutofautiana katika nyakati tofauti katika mzunguko wa hedhi, wakati wa ujauzito, na wakati wa mshawasha anapohitaji kushiriki ngono. Hata hivyo, uteute unapoongezeka au kuwa na harufu mbaya huwa ni dalili ya kuwepo maambukizi. Sababu kubwa zaidi ya tatizo hili ni maambukizi ya fangasi ambao husababisha kutokwa na uchafu kama jibini ya maziwa, na kuwashwa kuzunguka au ndani ya uke, na wakati mwingine maumivu wakati wa kukojoa. Aina hii ya maambukizi haiambukiziwi kwa njia ya ngono. Inasababishwa na hali ambazo zinapelekea ukuaji na kuongezeka kwa fangasi ukeni, kama vile kutumia antibiotiki kwa muda mrefu, kuvaa nguo zinazobana sana, na kusafisha uke kwa kuingiza vitu au kusugua sehemu ya ndani au kutumia marashi ukeni na msongo mkubwa wa mawazo. Baadhi ya uteute unaotoka ukeni unaashiria kuwa una ugonjwa wa ngono na unahitaji matibabu kutoka kwa daktari.
Mwone daktari kama
Panga kumwona daktari kama unadhani una ugonjwa wa ngono na/au:
- Uchafu unaotoka ukeni una damu au una rangi ya kijani-manjano, au kama unanuka vibaya
- Una dalili nyingine kama vile homa na maumivu sehemu ya chini ya tumbo
- Una tokwa na uchafu ukeni usio wa kawaida mara kwa mara
- Una ujauzito
Uchafu unatoka ukeni – unachoweza kufanya wewe mwenyewe
Kama una uhakika kuwa una maambukizi ya fanasi, unaweza kujitibu mwenyewe. Anza matibabu mapema iwezekanavyo unapoanza kuona dalili.
- Tumia dawa za kudhibiti fangasi ‘’antifungal. Dawa hizi zinatengenezwa kwa mifuo miwili. Unaweza kutumia ‘’clorimazole au ‘’miconazole’’ ambayo inaweza kuwa ya kidonge au ‘’cream’’.
- Aina hizi zote, unapaswa kuziweka ukeni ukiwa umelala chali, ili dawa isivuje au kudondoka.
- Ni vizuri kuziumia kabla ya kulala ili zifanye kazi usiku mzima
- Ili kupunguza karaha na mwasho, jaribu kuongeza ‘’baking soda kwenye maji ya kuoga. ‘’Baking soda’’ itasaidia kupooza na kuzuia usumbufu. Ongeza vijiko 2 kwenye maji ya uvguvugu na kisha jiloweka
Kuzuia
Kama unapata maambukizi ya fangasi mara kwa mara, mambo yafuatayo yatasaidia kupunguza kujirudia rudia
- Usivae nguo za ndani zinazobaa sana ‘’panyhose, ”panty liners”. Tumia ‘’pads’’ wakati wa damu ya hedhi
- Tumia maji pekee na sabani isiyokuwa na ‘’perfume au dawa unapokuwa ukisafisha uke
Mwone daktari kama
Panga kumwona daktari
- Maambukizi hayajaisha baada ya ufuata njia zilizozungumziwa hapa au baada ya kutumia madawa ya daktari