Ugonjwa sugu wa figo ni nini?
Ugonjwa sugu wa figo unatokea baada ya figo kuharibiwa na kusababisha zishidwe kusafisha damu au kufanya kazi yake vizuri. Asilimia 10 ya watu wote duniani wameathirika na ugonjwa wa figo. Ugonjwa wa figo unaweza kumkumba mtu wa umri wowote. Nusu ya watu wenye umri wa miaka 75 na zaidi wana ugonjwa sugu wa figo.
Figo zinafanya kazi gani?
Figo zinasafisha damu kwa kutoa taka mwili kwenye damu, ambazo huondolewa mwilini kupitia kwenye mkojo. Figo zina kazi muhimu ya kuweka uwiano wa vimiminika mwilini. Figo zinasaidia pia kudhibiti shinikizo la damu, kuweka imara mifupa, na kutengeneza seli nyekundu za damu.
Ni nini husababisha ugonjwa sugu wa figo?
Kuna sababu na mambo mengi yanayoweza kusababisha ugonjwa sugu wa figo. Sababu mbili kuu zinazosababisha ugonjwa sugu wa figo ni ugonjwa wa kisukari na shinikizo la juu la damu.
Ni zipi dalili za ugonjwa sugu wa figo?
Mwanzo wa Ugonjwa sugu wa figo huwa hauna dalili za mwanzo. Mtu anaweza kupoteza mpaka asilimia 90 ya uwezo wa figo zake kufanya kazi kabla hajaona dalili yoyote. Kwa Kama una ugonjwa sugu wa figo, unaweza ujisikie vizuri kama ilivyo kawaida. Unaweza kuwa na dalili zifuatazo:
- Uchovu
- Maumivu ya tumbo
- Udhaifu wa misuli
- Kupata mkojo kidogo
- Kuvimba kwa miguu
- Kuvimbwa kwa macho / kope za macho
- Kutetemeka (hasa mikono)
- Kupungua kwa uwezo wa kufikiri
- Kuchanganyikiwa
- Kuvuja damu kwenye mfumo wa chakula
Mambo yanayoongeza hatari ya kupata ugonjwa sugu wa figo
Mambo yafuatayo yanaongeza hatari ya kupata ugonjwa sugu wa figo:
- Kama una ugonjwa wa shinikizo la damu
- Kama unasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari
- Kama kuna historia ya ugonjwa sugu wa figo kwenye familia yenu
- Kama una uzito wa mwili uliokithiri
- Kama unavuta sigara
- Kama una umri wa miaka zaidi ya 50
Ukiwa na ugonjwa sugu wa figo ufanyiwe vipimo gani?
Kama una miaka 60 au zaidi, ni vizuri kuchunguzwa kama una ugonjwa wa kisukari, shinikizo la juu la damu, au kama una mwanafamilia mwenye ugonjwa wa figo. Daktari anaweza kuagiza ufanye vipimo ili kutathimini ugonjwa sugu wa figo. Atachunguza shinikizo lako la damu na kuagiza baadhi ya vipimo vya damu na mkojo ili kuangalia kama figo inasafisha vyema damu kwa kuangalia kiwango cha creatinine, na kuangalia kama kuna protini kwenye mkojo.
Unaweza kufanya nini ili kusaidia figo zako?
Ni vizuri kukaa mbali na vitu vinavyoweza kuharibu figo. Unapaswa:
- Kuacha kuvuta sigara
- Dhibiti kiwango cha sukari kwenye damu kama una ugonjwa wa kisukari
- Punguza shinikizo la damu ili kiwe katika kiwango salama kwa kupata mlo wa afya, mazoezi, na kutumia dawa
- Punguza kiwango cha mafuta / lehemu (cholesterol) kwenye damu
- Dhibiti uzito wa mwili
- Tumia dawa ili kupunguza kasi ya ugonjwa huu
- Epuka kutumia holela dawa zinazoitwa Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDS). Kwa mifano: ibuprofen na naproxen.
- Fanya mazoezi na jishushughulishe
Matibabu ya ugonjwa sugu wa figo
Bonyeza hapa kujifunza zaidi kuhusu: Figo kushindwa kufanya kazi yake
Angalizo
Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.