Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa brucella (brucellosis) ni ugonjwa wa kuambukizwa unatokana na kugusana na wanyama wenye maambukizi ya bakteria aina ya brucella.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa brucella?

Ugonjwa wa brucella unaanza na dalili kama za mafua, dalili kama vile:

Homa inaongezeka na kuwa kali sana nyakati za jioni. Joto la mwili linapatanda na kushuka kama mawimbi. Dalili nyingine ni pamoja na:

  • Maumivu ya misuli
  • Kuvimba kwa matezi

Ugonjwa huu unaweza kuwa sugu na kudumu kwa miaka mingi.

Ni nini husababisha ugonjwa wa brucella?

Bakteria wa brucella wanaweza kuambukiza ng’ombe, mbuzi, ngamia, mbwa na nguruwe. Bakteria huyu anaweza pia kuambukiza mwanadamu kama atakutana na nyama yenye maambukizi au kula au kunywa maziwa ambayo hayajatibiwa au jibini.

Ni nani yuko kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa brucella?

Watu wanaofanya kazi zinazohusisha kukutana na Wanyama au nyama, kama vile wachinjanji, wakulima au wataalamu wa wanayma, wako kwenye hatari zaidi.

Ni wakati gani unapaswa kutafuta matibabu haraka?

Onana na daktari kama:

  • Una dalili za ugonjwa wa brucella
  • Kama dalili zinaendelea kuongezeka au haujaanza kuona nafuu baada ya matibabu
  • Umeanza kuona dalili mpya

Utambuzi wa ugonjwa wa brucella

  • Kupandikiza damu ili bakteria waote kwa ajili ya utambuzi – blood culture
  • Kupandikiza uboho ili bakteria waote kwa ajili ya utambuzi – bone marrow culture
  • Vipimo vya kuangalia muitikio wa kinga mwili – serology for brucellosis antigen

Uchaguzi wa matibabu ya ugonjwa wa brucella

Dawa za antibiotiki hutumika kutibu maambukizi ya ugonjwa wa brucella na kuzuia ugonjwa usijirudie. Unaweza kupewa dawa kwa muda mrefu zaidi kama kuna matatizo yatasababishwa na ugonjwa huu.

Kuzuia

  • Kunywa au kula jibini au maziwa yaliyotibiwa ni njia muhimu sana ya kupunguza uwezekano wa kuambukizwa.
  • Watu wanaojishughulisha na kutunza au biashara ya nyama wanapaswa kuvaa miwani na nguo za kujikinga ili kuzuia maambukizi yasiingie kwenye vidonda.
  • Kuwatambua wanayama walioambukizwa ni muhimu. Kuna chanjo kwa ajili ya ng’ombe, na sio kwa ajili ya binadamu.

Matarajio?

Ugonjwa unaweza kujirudia, na dalili zinaweza kuwepo kwa maiaka mingi. Kama ilivyo kwa ugonjwa wa kifua kikuu, ugonjwa unaweza kujirudia baada ya muda mrefu.

Matatizo yanayoweza kutokea?

MAELEZO ZAIDI KUHUSU UGONJWA WA BRUCELLA

Maelezo ya jumla

Ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria, unaathiri mwili mzima na unaambukizwa kwa watu kutoka kwa wanyama

Sababu ya ugonjwa wa brucella

  • Brucella melitensis (hii ndio aina inayopatikana zaidi duniani), unasambaa kutoka kwa mbuzi, kondoo na ngamia
  • Brucella abortus kutoka kwa ng’ombe
  • Brucella suis kutoka kwa nguruwe
  • Brucella canis kutoka kwa mbwa

Epidemiolojia ya ugonjwa wa brucella

Inapatikana dunia nzima. Unawapata zaidi watu wanofanya kazi na kukutana na wanyama walioambukizwa au tishu hasa wafugaji, madaktari wa wanyama na wachinjaji wa wanayama, ambao wengi wao ni wanaume.

Milipuko inaweza kutokea kwa watu wanotumia maziwa mabichi au bidhaa zilizotengenezwa na maziwa mabichi, hasa jibini ya maziwa ya ng’ombe, kondoo na mbuzi.

Uambukizo wa ugonjwa wa brucella

Kwa kugusa tishu, damu, mkojo, majimaji ya ukeni, mtoto aliyetoka mimba ikiharibika na hasa mfuko wa uzazi/kondo – maambukizi yanapitia kwenye kiconda kwenye ngozi. Mara nyingi inatokea kwa kula maziwa mabichi na bidhaa za maziwa za wanyama walioambukizwa (nyama mbichi au uroto wa mifupa). Maambukizi yanaweza kutokea kwa njia ya hewa kwenye maabara na kwenye machinjio.

Muda kabla dalili kuanza

Inaweza kuchukua wiki 1-3 au inaweza kuwa miezi kadhaa

Muda wa uambukizi

Hakuna Ushahidi wowote kuwa maambukizi yanawea kutoka kwa mtu mmoja mpaka kwa mwingine

Nani yuko kwenye hatari

Ukali wa dalili na muda wa ugonjwa unatofautiana sana kati ya mtu na mtu. Uwepo wa kinga baada ya kupata maambukizi haufahamiki.

Dalili

  • Dalili zinaanza ghafla
  • Dalili za kawaida ni; homa, kutokwa jasho, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, uchovu, kichefuchefu, maumivu ya maungio na sehemu ya chini ya mgongo, kupungua uzito, kufunga choo, koo kuuma na kikohozi kikavu.
  • Katika uchunguzi wa mwili daktari anaweza kuona
  • Mara nyingi hakuna ishara yoyote nyingine, mgonjwa anaonekana poa
  • Wengine wanajihisi kuumwa, mtoki, kuvimba kwa wengu na ini, kuvimba kwa maungio, maumivu kwenye uti wa mgongo, upele kwenye ngozi, mapigo ya moyo yasiyosawa au nimonia

Utambuzi

  • Historia ya kukutana na nyama au mnyama mgonjwa na dalili
  • Kwa kupima damu – serology – raised B. agglutini
  • Kupandikiza sampuli – culture of bloo/bone marrow

Matibabu

  • Doxycyline + aminogrycoside kwa wiki 2 ikifuatwa na Doxycycline + Rifampcin kwa wiki 4-8

Kuzuia

  1. Kuzuia kunategemea kukomesha ugonjwa kwa wanyama wanaofugwa
  2. Toa elimu ili watu wasinye maziwa mabichi au kula bidhaa za maziwa yasiyotibiwa
  3. Toa elimu katika sehemu za machinjio kuhusu hatari ya kuambukizwa ugonjwa huu
  4. Elimisha wawindaji kuhusu kutumia vifaa vya kujkinga (glavu na nguo)
  5. Ondoa wanyama walioambukizwa
  6. Tibu maziwa; pika nyama na mifupa vzr
  7. Tupa sehemu sahihi kondo, majimaji au kijusi cha mimba iliyotoka. Takasa maeneo yaliyochafuliwa.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000597.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *