Ugonjwa wa dondakoo ni nini?
Dondakoo (Diptheria) ni ugonjwa unaowapata watoto wadogo. Ugonjwa huu unasababishwa na vimelea ambavyo hujulikana kama “corynebacterium diphtheria” Vimelea hivi hushambulia sehemu za koo na huenezwa kwa njia ya hewa, mate au majimaji yanayotoka kwenye sehemu za maambukizo.
Ni zipi dalili za ugonjwa wa donda koo?
Ugonjwa wa dondakoo unaojionyesha kwa dalili zifuatazo: –
- Kukosa hamu ya kula na kushindwa kula
- Vidonda kooni
- Kutoa kamasi iliyochanganyika na damu
- Utando kwenye koo ambao humzuia mtoto kumeza na hata kupumua
- Maumivu makali ya shingo
- Shingo pia huweza kuvimba sana na kupewa jina la ‘shingo ya nyati’. Hali hii inawza isitofautishwe na matumbwitumbwi.
Athari za ugonjwa wa dondakoo
- Ugonjwa huenea haraka sana
- Kushindwa kumeza na kupumua
- Mtoto anaweza kupooza sehemu za paji la uso hadi shingoni
- Kifo huweza kutokea
Kuzuia ugonjwa wa dondakoo
Dondakoo huzuiwa kwa chanjo yenye mchanganyiko wa chanjo za kuzuia Kifaduro, Pepopunda, Homa ya ini, Homa ya uti wa mgongo na kichomi yaani DTP- HepB-Hib ambayo kwa sasa hujulikana kama Pentavalent.
Ratiba ya chanjo
- Chanjo ya kwanza – Umri wa wiki sita
- Chanjo ya pili – Umri wa wiki kumi
- Chanjo ya tatu – Umri wa wiki kumi na nne
Matibabu ya ugonjwa wa dondakoo
Ugonjwa wa Dondakoo unatibika endapo mtoto atapata huduma mapema
Jifunze zaidi hapa – RATIBA YA CHANJO KWA WATOTO TANZANIA
Ujumbe muhimu
- Ujumbe huu huzuilika kwa chanjo
- Mpeleke mtoto katika Kituo cha Huduma za Afya akapate chanjo.
- Hakikisha mtoto amekamilisha sindano tatu kwa utaratibu uliowekwa ili apate kinga kamili.
- Baada ya matibabu, mpumzishe mtoto kitandani kwa muda wa wiki sita, ili apate nguvu za kutosha.
MAELEZO ZAIDI KUHUSU UGONJWA WA DONDAKOO
Maelezo ya jumla
Ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria unaosababisha matatizo kwenye tonsils, koo, pua, na kwa mara chache kwenye shemu nyingine zote zilizofunikwa na utando ute au ngozi na kwa mara chache jicho au via vya uzazi.
Sababu ya dondakoo
Coynebacterium diptheriae
Epidemiolojia ya ugonjwa wa dondakoo
Ni ugonjwa wa wakati wa baridi, unawapata zaidi watoto ambao hawajapata chanjo wenye umri chini ya mika 15. Ni kawaida kuupata ugonjwa huu kwa watu wazima ambao hawakupata chanjo walipokuwa watoto. Visa vya dondakoo visivyo na dalili yoyote, vyenye dalili kwenye ngozi na vidonda zipo sana katika maeneo haya yetu ya kitropiki.
Uambukizo wa dondakoo
Kukutana na mgonjwa. kwa mf: kukutana na majimaji ya kinywa au pua au ngozi iliyaothirika
Muda kabla dalili kuanza
Kwa kawaida ni sku 2-5
Muda wa uambukizo wa dondakoo
Inategemea, mpaka bakteria akiondoka kabisa kwenye majimaji na vidonda; kwa kawaida ni baada ya wiki 2 au chini ya hapo.
Nani yuko kwenye hatari
Mtu yoyote anaweza kuambukizwa. Watoto wachanga waliozaliwa na kinamama wenye kinga hurithi kinga kiasi, lakini ulinzi huisha baada ya miezi 6. Kupona baada ya kuugua sio mar azote kunakupatia kinga ya maisha. Unaweza kupata kinga ya kudumu kwa kupata chanjo diptheria toxoid.
Dalili za ugonjwa wa dondakoo
- Ukiangalia kupitia kooni, unaona utando wa kahawia ukiwa umegandia kwenye sehemu ya nyuma ya koo ukizungungwa uvimbe – pseudo membrane
- Kunakuwa na maumivu ya koo, tezi za shingo zinaweza kuwa zimevimba na kuuma; katika hali kali, kunaweza kuwepo uvimbe unaonekana kwenye shingo
- Ishara nyingine zinaweza kuchelewa na kutokea wiki 2-6 baada ya maambukizi, matatizo ya mfumo wa fahamu na moyo (kuvimba kwa misuli ya moyo)
Utambuzi wa ugonjwa wa dondakoo
- Kwa kuangalia dalili na epidemioljia
- Kuchunguza kama kuna bakteria kwenye majimaji yanayotoka kwenye uvimbe
Matibabu ya dondakoo
- Dawa ya kuzuia sumu ya diptheria – diptheria antitoxin
- Erythromycin kwa wiki 2 lakini wiki 1 kwa ugonjwa unaothiri ngozi
- Procaine penicillin kwa siku 14 au dozi moja ya Benzathin penicillin
Lengo kuu la matibabu ni kuonda kabisa C. diptheriae na kuzuia maambukizi kwenda kwa watu wengine
Kuzuia
- Elimisha umma, hasa wazazi kuhusu matatizo yanayoweza kuletwa na dondakoo na umuhimu wa chanjo
- Wapatie chanjo watoto – diptheria toxoid
- Safisha maeneo na vitambaa vyenye majimaji ya mgonjwa
- Dozi moja ya sindano za penicillin (IM) au dawa za kumeza za erythromycin kwa siku 7-10 zinashaueiwa kwa watu waliokutana na mgonjwa wa dondakoo