Maelezo ya jumla
Ugonjwa wa ekinokokasi (hydatid disease/echinococcosis) ni ugonjwa unaosababishwa na minyoo aina ya tegu anayeitwa Echinococcus glanusus.
Sababu ya ugonjwa wa ekinokokasi
Echinococcus granulosus, mnyoo aina tegu anayepatikana kwa mbwa
Epidemiolojia ya ugonjwa wa ekinokokasi
Unatokea katika mabara yote isipokuwa Antarctica. Unapatikana zaidi katika nchi yenye uchungaji wa wanyama ambapo mbwa wanakula nyama yenye mayai.
Mbwa wa kufugwa na jamii zake ndio wahusika zaidi; wanabeba maelfu ya minyoo ya tegu kwenye utumbo wao bila kuwa na dalili zote. Kondoo pia wanahusika kwa sehemu yao.
Umbukizo
Moja kwa moja kwa kuchukua mayai kwenye mikono na kuweka mdomoni baada ya kucheza na mbwa mwenye maambukizi au kupitia chakula, maji, au udongo uliochafuliwa
Muda kabla ya dalili kuanza
Inategemea, kuanzia miezi 12 mpaka miaka kadhaa, inategemea na namba na sehemu uvimbe (cyst) na ni kwa kasi kiasi gani utakua.
Muda wa uambukizo ya ugonjwa wa ekinokokasi
Mbwa walio na maambukizi wanaanza kupitisha mayai wiki 7 baada ya maambukizi. Karibia maambukizi ya wanyama wote aina ya Mbwa wanapona hata bila matibabu baada ya miezi 6.
Nani yuko kwenye hatari zaidi
Watoto wako kwenye hatari zaidi kupata maambukizi kwa sababu wanacheza zaidi na mbwa
Dalili za ugonjwa wa ekinokokasi
- Dalili na ishara zinatofautiana kulingana na sehemu na namba ya cyst zinazotengenezwa
- Kupasuka au kutoboka kwa cyst kunaweza kusababisha mtu kupata mzio mkali sana
- Kwa kawaida cyst ni mviringo, zina ukuta mpana na kwa mara nyingi zinapatikana kwenye ini au mapafu
Utambuzi wa ugonjwa wa ekinokokasi
- Historia ya kuishi eneo lenye ugonjwa huu na ukaribu na mbwa
- Kwa kupiga picha ya ekisirei na Ct scan
- Kwa kufanya kipimo cha damu – serologic test
Matibabu ya ugonjwa wa ekinokokasi
- Kwa kufanyiwa upasuaji kuondoa cyst zilizopo
- Albendazole (mebendazole)
- Kama cyst ikipasuka, praziquatel
Kuzuia
- Elimisha umma kuepuka kukutana na kinyesi cha mbwa. Kunawa mikono kusisitizwe.
- Zuia maambukizi kwa mbwa, kwa huzuia mbwa kula nyama ambayo haijapikwa
- Utupaji salama wa nyama au viungo vya wanyama walio na maambukizi
- Kutoa tiba mara kwa mara kwa mbwa walio kwenye hatari ya kuambukizwa