Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa giardiasis ni maambukizi ya protozoa anayekaa kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo yanayosababisha kuharisha sugu, maumivu ya tumbo, kujaa kwa tumbo, uchovu, kuharisha kinyesi chenye mafuta na kupungua uzito

Sababu za giardiasis

Giardia lamblia

Epidemiolojia ya giardiasis

  • Unatokea duniani kote.
  • Watoto wanapatwa zaidi na maambukizi ukilinganisha na watoto
  • Ugonjwa huu unapatikana zaidi kwenye maeneo yanye usafi duni

Umbukizo wa ugonjwa wa giardiasis

Maambukizi yanatokea kati ya mtu na mtu kupitia mikono iliyo shika kinyesi na mayai kubakia kwenye mikono

Kipindi cha uambukizo wa ugonjwa wa giardiasis

Kipindi chote cha uambukizo, mara nyngi ni miezi

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata giardiasis

  • Watu wenye maambukizi ambao hawana dalili ni wengi
  • Mara nyingi ugonjwa huu unapona wenyewe bila matibabu kwa watu wengi
  • Watu wenye ugonjw wa UKIMWI hupata dalili kali na za muda mrefu zaidi

Ugonjwa wa giardiasisMchakato wa uambukizo – life cycle

  1. Unapokunywa au kula chakula kilichochafuliwa na mayai
  2. Mayai yanaanguliwa tumboni na kutoa vilimbwende vinavyoitwa trophozoites
  3. Trophozoites zinazaliana na kuongezeka tumboni
  4. Trophozoites zinajitengenezea gamba na kuwa yai
  5. Mayai yanatoka nje kwenye kinyesi
  6. Kinyesi chenye maai kinachafua mazingira tayari kwa uambukizo

Dalili za giardiasis

  • Dalili zinaweza zisiwepo au zinaweza kusababisha mtu akaugua sana na kushindwa kufyonza vizuri chakula
  • Watoto wadogo kwa kawaida wanahara lakini mara nyingi tumbo linavimba na kujaa
  • Watu wazima wana maumivu ya tumbo, kuhara, kichefuchefu, uchovu na kujaa tumbo

Utambuzi wa ugonjwa wa giardiasis

  • Kuwepo kwa mayai a Giardia lamblia au trophozoite kwenye kinyesi

Matibabu ya giardiasis

Metronidazole au Tinidazole

Kuzuia ugonjwa wa giardiasis

  1. Usafi binafsi na kunawa vizuri mikono kabla ya kulan a baada ya kutumia choo
  2. Matumizi sahihi ya choo
  3. Kulinda vyanzo vya maji vizichafuliwe na kinyesi
  4. Kutibu wagonjwa mapema
  5. Kuwa na chanzo salama cha maji

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000288.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *