Maelezo ya jumla
Ugonjwa wa homa ya manjano (yellow fever) ni ugonjwa unaoambukizwa na mbu. Ugonjwa huu unapatikana zaidi Amerika ya kusini na kusini mwa jangwa la Sahara Afrika.
Ni zipi dalili za ugonjwa wa homa ya manjano?
Dalili ni pamoja na:
- Kuvurugika kwa mapigo ya moyo, moyo kuanza kushindwa kufanya kazi vizuri
- Kuvuja damu (ugonjwa unaweza kuendelea mpaka kusababisha ukaanza kuvuja damu)
- Koma
- Kupungua kwa kiasi cha mkojo unachopata
- Unaanza kujihisi kuchanganyikiwa
- Homa
- Maumivu ya kichwa
- Manjano kwenye ngozi na macho na sehemu ya ndani ya mdomo
- Maumivu ya misuli
- Macho mekundu, uso mwekundu, ulimi mwekundu
- Degedege
- Kutapika
- Kutapika damu
Ni nini husababisha ugonjwa wa homa ya manjano?
- Ugonjwa wa homa manjano unasababishwa na kirusi anayesamabzwa kwa kuumwa na mbu. Ugonjwa huu unapatikana zaidi Amerika ya kusini na kusini mwa jangwa la Sahara.
- Ugonjwa wa homa ya manjano una hatu tatu:
-
- Hatua za awali: Maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli na viungo, homa, kutokwa na kijasho chembamba, kupungua kwa hamu ya chakula, kutapika, na kuwa na njano kwenye ngozi, ulimi au macho. Hii hutokea kama siku 3 – 4, mara nyingi dalili hizi hupotea kwa muda .
- Kipindi kisicho na dalili: Baada ya siku 3-4, homa na dalili nyingine hupotea. Watu wengi hupona katika hatua hii, lakini wengine wanaweza kuingia katika hatua ya hatari ya tatu ndani ya masaa 24.
- Hatua hatari ya tatu: Kuharibika kwa viungo mbalimbali vya mwili. Hii ni pamoja na moyo, ini, na figo, unaanza kuvuja damu, damu inashindwa kuganda, na ubongo unashidwa kufanya kazi, unaanza kujihisi kuchanganyikiwa, degedege, koma, mshtuko na hatimaye kifo
Nani yuko kwenye hatari zaidi?
Mtu yeyote anaweza kupata ugonjwa wa homa ya manjano, lakini wazee wako kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa mkali. Kama mtu ameumwa na mbu mwenye maambukizi, dalili kwa kawaida zinaanza kuonekana baada ya siku 3 – 6.
Ni wakati gani napaswa kutafuta matibabu haraka?
Mtu mwenye ugonjwa mkali atakuwa na dalili za kuonesha kuwa ini, figo na moyo umeanza kushindwa kufanya kazi. Ongea na daktari haraka sana kama wewe au mtoto ana homa, maumivu ya kichwa, kutapika, au manjano, hasa kama unaishi au umesafiri kwenda kwenye eneo lenye mlipuko wa homa ya manjano. Vipimo vya damu vitahakikisha utambuzi wa ugonjwa wa homa ya manjano.
Utambuzi wa ugonjwa wa homa ya manjano
- Mtu mwenye ugonjwa mkali atakuwa na dalili zinazoonesha kuwa ini, figo na moyo vimeanza kushindwa kufanya kazi
- Vipimo vya damu vitahakikisha utambuzi wa ugonjwa wa homa ya manjano kwa kuangalia utendaji kazi wa ini, figo na moyo.
Uchaguzi wa matibabu ya ugonjwa wa homa ya manjano
Hakuna matibabu mahususi kwa ajili ya ugonjwa wa homa ya manjano. Madaktari hujikita katika kudhibiti na kutibu dalili zilizopo ili kuupatia mwili nafasi ya kupambana na virusi waliomo mwilini.
- Utaongezewa damu kama una vuja damu sana
- Damu yako itasafishwa kwa mashine (dialysis) kama figo zimepata shida
- Utaongezewa maji mwilini kupitia kwenye mishipa
Matarajio ukiwa na ugonjwa wa homa ya manjano
Ugonjwa wa homa ya manjano unatofautianakwa ukali kati ya mtu mmoja na mwingine. Watu wachache wanaopata ugonjwa mkali unaosababisha kuvuja damu – karibia nusu hufa kutokana na ugonjwa huu.
Matatizo yanayoweza kujitokeza
- Koma
- Kifo
- Tatizo linalosababisha kuvuja damu bila kusimama – unavuja damu kupitia matundu yote ya mwili
- Kushindwa kwa figo kufanya kazi
- Kushindwa kwa ini kufanya kazi
- Kuvimba kwa matezi mdomoni
- Kupata maambukizi
- Kushindwa kwa moyo kufanya kazi yake
Kuzuia ugonjwa wa homa ya manjano
Kuna chanjo inayofanya kazi kwa ufanisi mkubwa dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano. Ni vizuri kufika kituo cha afya angalau siku 10 – 14 kabla ya kusafiri kwenda eneo lenye mlipuko au linalojulikana kuwa na ugonjwa wa homa ya manjano ili kujua kama utahitaji kupewa chanjo dhidi ya ugonjwa huu
Kama utasafiri kwenda eneo lenye mlipuko au linalojulikana kuwa na ugonjwa wa homa ya manjano, fanya yafutayo
- Lala ndani ya nyumba yenye madirisha yaliyotiwa wavu au yaliyokingwa vizuri
- Tumia dawa za kufukuzia mbu
- Vaa nguo zinazokufunika vizuri, shati za mikono mirefu, suruali ndefu, kofia , n.k.
MAELEZO ZAIDI KUHUSU HOMA YA MANJANO
Maelezo ya jumla
Ni maambukizi yanayosababishwa na virusi yanayosababisha dalili kwa muda mfupi na kwa makali tofauti tofauti.
Sababu
Virusi vya yellow fever
Epidemiolojia
- Homa ya manjano inakadiriwa kusababisha visa 200000 na vifo 30,000 kila mwaka, 90% vikitokea barani Afrika.
- 20% mpaka 50% ya watu walioambukizwa wanaopata ugonjwa mkali hufa
Umbukizo
Kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes aegypti mwenye maambukizi
Muda kabla dalili kuanza
Siku 3-6
Muda wa uambukizo
Damu ya mwanadamu inakuwa tayari kumwambukiza mbu muda mchache kabla ya homa kuanza na kwa siku 3-5 za ugonjwa. uambukizo ni mkubwa zaidi katika eneo lenye mbu wengi na watu wengi walio hatarini.
Nani yuko kwenye hatari
Kupona baada ya kuumwa ugonjwa wa homa ya manjano kunakuacha na kinga; Kuguua mara ya pili sio kitu kinachowezekana. Watoto wanaozaliwa na kina mama walio na kinga wanapata kinga muda ambayo inaweza kudumu kwa muda wa miezi 6. Baada ya kuambukizwa, kinga inatengenezeka ndani ya wiki ya kwanza.
Dalili
- Maambukizi ya kawaida huanza na homa, kutetemeka, maumivu ya mgongo, maumivu ya mwili, uchovu, kichefuchefu na kutapika
- Kuvuja damu ni kawaida kwenye pua, kwenye fizi, kutapika damu, na kupata kinyesi cha damu
- Manjano inatokea kwa sababu ya kuharibiwa kwa seli za ini na hii inaweza kusababisha kushindwa kwa ini na hata kifo
- Kupoteza protini (albumin) kwenye mkojo kunatokana na kuharibiwa kwa seli za figo na hii inaweza kusababisha kushindwa kwa figo
- Wagonjwa wanaoishi mpaka siku ya 7 ya ugonjwa mara nyingi wanapona
Utambuzi
- Kuangalia historia ya mgonjwa anapoishi au kama amesafiri kwenda eneo lenye maambukizi
- Dalili
Matibabu
Hakuna matibabu ya moja kwa moja – daktari hujaribu kushughulika na kila dalili ianayojitokeza
Kuzuia
- Kutoa chanjo kwa watu wote wenye umri zaidi ya miezi 9 kama wanaishi, wanafanya kazi au wanasafiri kwenda maeneo hatari
- Kudhibiti mbu aina ya Aedes aegypti katika maeneo ya mijini
- Kutoa taarifa kwa vyombo husika kama unadhani kuna mlipuko
Vyanzo
https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a607030.html