Ugonjwa wa homa ya nyani ni nini?

Homa ya nyani (monkeypox) ni ugonjwa unaosababishwa na virusi uliogunduliwa kwa nyani waliokuwa wamelelewa maabara mwaka 1958. Ugonjwa huu unapatikana zaidi katika nchi za magharibi mwa Afrika. Aina nyingi za wanyama ikiwemo na binadamu wanaweza kuambukizwa ugonjwa huu. Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa mpox vinafanana kwa karibu na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ndui (smallpox) na ugonjwa wa homa ya ng’ombe (cowpox) kwa wanadamu.

Ni wanyama gani wanaweza kuambukizwa ugonjwa wa homa ya nyan?

Nyani, jamii zote za panya (panya wa nyumbani, panya buku, kichakuro, kindi) na sungura wanaweza kuambukizwa ugonjwa huu. Ukweli ni kuwa, hatujui kwa hakika aina zote/ gani na gani za wanyama wanaweza kuambukizwa virusi hawa. Yawezekana wapo wanyama wengine wa mwituni au wa kufuga wanaoweza kuambukizwa lakini hatuwajui bado.

Wanyama wanaambukizwaje ugonjwa wa homa ya nyani

Ugonjwa wa homa ya nyani unasambaa kwa kugusana moja kwa moja na mnyama aliyeambukizwa. Hii inaweza kutokea kupitia vidonda kwenye ngozi au majimaji kwenye hewa.

Wanyama wanaathiriwa vipi na ugonjwa wa homa ya nyani

Kwa wanyama wa jamii ya nyani, kwa kawaida ugonjwa wa homa ya nyan unajitokeza kama upele unaodumu kwa siku 4 mpaka wiki 6; malengelenge yaliojaa usaha yataonekana mwili mzima, lakini yatakuwa mengi zaidi kwenye uso, miguu, viganja vya mikono, nyayo za miguu na mikia. Ni nadra sana kifo kutokea, isipokuwa kwa nyani wachanga. Baadhi ya nyani wanaweza kuambukizwa virusi hawa na wasipate dalili zozote.

Wanadamu wanaambukizwaje ugonjwa wa homa ya nyanii

Watu wanaweza kuambukizwa ugonjwa wa homa ya nyan kwa kugusana moja kwa moja na damu, majimaji ya mwili na vidonda vya mnyama aliye na uambukizo. Dalili za ugonjwa zinaanza kuonekana kuanzia siku ya 12 baada ya kuambukizwa. Dalili hizi ni pamoja na;

Baada ya siku 1 mpaka 3 upele mkubwa unaanza kutokea kwenye mikono na miguu na hata usoni au kwenye mwili. Baadae mapele haya yanabadilika na kuwa kama majipu au malengelenge yaliyojaa usaa. Katika hatua za mwisho, yanapasuaka na kukauka na mwisho yanatawanyika. Ugonjwa huu unadumu kwa muda wa wiki 2 mpaka 4 na watu wengi wanapona vizuri tu.

Nifanye nini kama ninashuku kuwa nina ugonjwa wa homa ya nyani?

  • Kwa mnyama – ongea/ mpigie mtaalamu wa wanyama haraka
  • Kwa mwanadamu – Ongea / mpigie daktari haraka inavyowezekana

Nitawalinda vipi wanyama wangu na ugonjwa wa homa ya nyan

Kuwapatia chanjo ya vaccinia (ni chanjo inayotumika kukinga dhidi ya ugonjwa wa ndui) inaweza kuwakinga wanyama jamii ya nyani na ugonjwa wa homa ya nyan. Kwa wanyama wengine njia nzuri ya kuwakinga ni kuhakikisha hawakutani na wanyama au watu wenye maambukizi.

Nitajilinda vipi na ugonjwa wa homa ya nyani?

Jitahidi usikutane na wanyama au watu walioambukizwa virusi vya homa ya nyanii.

  • Epuka kuchangia vitu kama nguo na matandiko ambavyo vimetumiwa na mtu mwenye dalilo za mpox
  • Epuka kugusana kwa kupeana mikono, kubusiana, kukumbatiana au kujamiiana na mtu mwenye dalili za mpox
  • Epuka kugusa majimaji ya mwili ya mtu mwenye dalili za mpox
  • Epuka kumbudumia mgonjwa mwenye dalili za mpox bila kuchukua tahadhari
  • Nawa mikono mara kwa mara na maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono

Japo chanjo inayotumika kukinga ugonjwa wa ndui (smallpox) inaonekana inaweza kufanya kazi kukinga watu dhidi ya homa ya nyani.  Inapendekezwa itumiwe na watu wanaoshiriki moja kwa moja kuuchunguza na kuudhibiti ugonjwa wa homa ya nyan, au wanaofanya tafiti na chunguzi mbalimbali za moja kwa moja kuhusu ugonjwa huu. Chanjo inaweza kutolewa mpaka siku 14 baada ya kuambukizwa.

Vyanzo

http://www.cdc. gov/ncidod/monkeypox/

 

Shares:
5 Comments
  • Dr Mniko
    Dr Mniko
    June 12, 2022 at 10:37 pm

    Asante

    Reply
  • Dr Eliachim
    Dr Eliachim
    March 11, 2025 at 2:31 am

    Asante kwa elimu nzuri

    Reply
  • keilyn
    keilyn
    March 12, 2025 at 4:08 pm

    Asante kwakutupa mwangaza wahili jambo

    Reply
    • DrMniko
      March 13, 2025 at 8:13 am

      Karibu sana, endelea kutufuatilia. Tusaidie kusambaza jumbe zetu pia.

      Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *