Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo ni nini?

Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo ni maambukizi au uvimbe unaotokea kwenye utando mdogo unaofunika ubongo na uti wa mgongo. Unaweza kusababishwa na maambukizi, dawa au kansa/saratani.

Ni zipi dalili za homa ya uti wa mgongo?

Unaweza kujisikia shingo inauma, una homa, maumivu ya kichwa, na uchovu kwa ujumla. Baadhi ya watu wanajihisi kuchanganyikiwa, au kuchoka sana.

Watoto hawatulii (wanahangaika/kulia sana), wanaweza kuwa na usingizi mzito sana/kulala sana, mwili unaweza kuwa umejikaza, au wanakula kidogo kuliko ilivyo kawaida.

Nani anaweza kupata ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo?

Mtu yeyote anaweza kupata ugonjwa huu, ila unawapata zaidi watoto walio na umri chini ya mwaka mmoja na watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 60. Unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa kukohoa, na hii ndio sababu vijana wadogo wanaoishi kwenye mambweni au hostel wako kwenye hatari zaidi ya kuupata. Unaweza pia kupata ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo kwa kubusu au kunywa kinywaji cha mtu aliyeambukizwa.

Ugonjwa huu unatambuliwa vipi?

Daktari atakuuliza maswali na kufanya uchunguzi wa mwili. Kama daktari anadhani kuwa una ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo, utahitajika kufanyiwa vipimo. Katika hospitali, utahitaji kufanyiwa vipimo vya damu na kipimo cha majimaji ya uti wa mgongo. Kipimo hiki kinachoitwa “lumbar puncture” kinahusisha kutoboa sehemu ya uti wa mgongo kwa kutumia sindano na kutoa majimaji kwa ajili ya kuyapima. Majimaji haya yatasaidia kujua kama una maambukizi. Yatasaidia pia kujua ni aina gani ya maambukizi uliyonayo. Wakati mwingine utahitaji kufanyiwa kipimo cha CT scan ili kupiga picha za kichwa.

Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo unatibiwa vipi?

Kama ni bakteria au fangasi ndio wamesababisha maambukizi, basi hali ni hatari. Utapaswa kubakia hospitalini ili kutibiwa kwa dawa za kuwekwa kwenye mishipa ya damu (IV) na sio vidonge. Utapaswa kupewa dawa hizi kwa ngalau wiki nzima au zaidi. Itachukua siku kadhaa kwa hali kuimarika ili uweze kuruhusiwa kwenda nyumbani. Kama ugonjwa unasababishwa na virusi, unaweza kupata nafuu hata bila kutumia dawa. Daktari atazungumza nawe kuhusu aina ya maambukizi uliyonayo.

Nini cha kutarajia kama una ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo?

Watu wengi hupona kama ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo utatibiwa. Baadhi ya watu wazima wanapatwa na degedege, kudhoofika kwa mkono au mguu, au matatizo mengine ya mfumo wa fahamu. Karibu 5% mpaka 15% ya watu wanaopata maambukizi makali hufa.

Ufanye nini kuzuia ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo?

Pata chanjo zote unazopaswa kupata. Kama hauzifahamu muulize daktari wako. Epuka kuwa karibu, kama vile kubusiana au kuchangia vikombe au vyombo vingine vya kula na mtu mwenye ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo. Kama uko karibu na mtu mwenye ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo, unaweza kupewa dawa ili kujikinga. Ongea na daktari na umwambie kuwa uko au ulikuwa karibu na mtu aliyetambuliwa kuwa na ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo

MAELEZO ZAIDI KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA UTI WA MGONGO

Maelezo ya jumla

Ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria unaosababisha kuvimba kwa utando unaofunika uti wa mgongo na ubongo

Sababu

Neisseria meningitides (meningococcus)

Epidemiolojia

Unatokea kwa wingi wakati wa baridi. milipuko inatokea kwa nadra. Inawapata zaidi watoto na vijana. inawapata zaidi watu wanaoishi katika mazingira ya msongamano

Uambukizo

Kukutana na matone ya majimaji yanayotoka kwenye pua au koo la mtu aliyeambukizwa

Muda kabla dalili kuanza

SIku 2-10, kwa kwaida siku 2-4

Muda wa uambukizo

Mtu ataendelea kuambukiza wengine kama bado kuna bakteria kwenye majimaji yanayotoka puani au kooni

Nani yuko kwenye hatari

Hatari ya kupata ugonjwa huu ni ndogo sana na kadri umri unavyoongezeka ndivyo na hatari inapungua

Dalili

  • Homa kali, maumivu makali ya kichwa, kichefuchefu na kutapika mara kwa mara, kukaza kwa shingo na kuwa na upele wa rangi ya pink kama damu imevilia chini ya ngozi.
  • Mgonjwa anahisi maumivu y mgongo kama moja ya mguu utakunjwa kwenye goti na kunyooshwa kuelekea juu – kernig’s sign

    Kernigs signs
    Kernigs signs
  • Shingo ya mgonjwa inapokunjwa, miguu inajikunja au inanyanyuka juu – Brudinski’s sign

    Brudzinski Sign
  • Kuanza kutokujitambu na koma

Utambuzi

  • Kwa kuangalia dalili na epidemiolojia
  • Kiwango cha seli nyeupe zinaongezeka kwenye damu – neurophils
  • Kuchukua majimaji kwenye mgongo na kuyachunguza -gram stain, WBC

Matibabu

  1. Ili kutibu mgonjwa, daktari hutoa dozi kubwa ya Crystalline penicillin kwenye mishipa
  2. Dawa ya kupunguza homa

Kuzuia

  1. Elimisha jamii kuhusu umuhimu wa kupunguza uweekano wa kukutana na majimaji yanayotoka kwa wagonjwa
  2. Punguza msongamano kazini, shuleni, kambi n,k
  3. Pata chanjo zinazopaswa (for strain A, C na Y strain0
  4. Patia matibabu wagonjwa
  5. Ptia dawa watu waliokutana na wagonjwa – chemoprophylaxis -mf; Rifampin kwa siku 2
  6. Toa taarifa kwa mamlaka zinazohusika

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000680.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *