KMaelezo ya jumla
Ugonjwa wa kichocho ni ugonjwa unaosababishwa na minyoo bapa aina ya trematode inayoishi kwenye mishipa ya damu ya mensenteric tumboni na kwenye kibofu kwa muda wa miaka mingi.
Sababu za ugonjwa wa kichocho
Aina kuu wadudu inayosababisha ugonjwa kichocho kwa wanadamu ni;
- Schistosoma mansoni
- Schistosoma Japonicum
- Schistosoma Hematobium
Kuna aina zingine zinazopatikana katika maeneo mengine machach ni pamoja na S. mekongi, S. intercalatum, S. malayesis, S. mattheei.
Aina zinazosababisha matatizo zaidi Afrika ni S. mansoni and S. hematobium.
Konokono ndio hubeba wadudu hawa wanaosababisha kichocho, kuna aina kuu 3 zinazohusika zaidi;
- Konokono aina ya Bulinus – S. hematobium
- Konokono aina ya Biomphalaria – S. mansoni
- Konokono aina ya Onchomelania – S. japonicum
Epidemiolojia ya ugonjwa w kichocho
Mansoni inapatikana zaidi Amerika kusini, visiwa vya karibea, Afrika na Mashariki ya kati. S hematobium inapatikana Africa na Mashariki ya kati. S. japonicum inapatikana magharibi ya mbali.
Ugonjwa huu unapatikana duniani kote na watu milioni 240 wanaambukizwa (WHO); Lakini wengi wa watu walioambukizwa wanapata dalili kidogo au hawapati dalilo kabisa, ni watu wachache tu wanaopata dalili kali. nWatu milioni 700 wanaishi kwenye maeneo hatarishi ote duniani
Uambukizo ya ugonjwa wa kichocho
Mtu anapata maambukizi kwa kukanyaga maji yenye mabuu wanaoitwa cercariae ambao wametengenezwa na kukua kutoka kwa konokono.
Muda kabla dalili kuanza
Unaweza kuonza kuwa na homa wiki 2-6 baada ya maambukizi. Maambukizi kwa binadamu yanaweza kudumu mpaka miaka 10. Konokono wanaendela kutoa mabuu (cercariae) katika kipindi choche wanachoishi (wiki kadhaa mpaka miezi 3)
Nani yuko kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa kichocho
Mtu yeyote anaweza kuambukizwa. Haifahamiki vyema kama kuna watu wenye kinga dhidi ya kichocho
- Namna ya uambukizo
-
- Mabuu aina ya cercariae yanatoboa ngozi na kuingia ndani kama umekanyaga maji yenye maambukizi
- Mabuu haya cercaria au schistosomula husafiri mpaka kwney mapafu na ini
- Mabuu yanakua na kuwa minyoo bapa (flukes) kwenye mishipa ya vena ianayotwa portal
- Minyoo hii bapa inasafiri na kujishikiza kwenye tumbo au kwenye kibofu cha mkojo kama ni s. haematobium
- Mayai yanayozaliwa kwenye vishipa vidogo yanachimba na kuingia kwenye utumbo au kwenye kibofu kama ni s. haematobium
- Mayai yanatolewa nje kwenye kinyesi au kwenye mkojo kama ni s. haematobium
- Mayai yanapofika kwenye maji yanaanguliwa na kutoa mabuu wanaitwa miracidia
- Miracidia wanaingia kwa konokono na kuzaliana kutengeneza mayai ambayo baadae huanguliwa kutengeneza mabuu yanaiitwa cercariae
- Mabuu ya cercariae yanaondoka kwa konokono na kuanza kuogelea kwenye maji tayari kuambukiz watu
Dalili ya ugonjwa wa kichocho
Kuna hatua kuu nne za ugonjwa wa kichocho
- Kumbukizwa
-
- Mabuu ya cercarie yanatoboa ngozi na kuingia
- Sehemu alipoingilia panawasha, panavimba
- Mabuu ya cercarie yanabakia kwenye ngozi kwa siku 5 kabla ya kuingia kwenye mfumo wa limfu na kufika kwenye ini
- Ukuaji
-
- Wadudu wa kichocho wanakua kwenye ini
- Homa, maumivu ya tumbo na kuwashwa (katayama syndrome)
- Minyoo inashuka kupita mshipa wa vena uanoitwa portana. s. mansoni wansafiri kwenda kwenye vena za tumboni na s, hematobium kwenda kwenye vena za kibofu cha mkojo
- Hatua hii inaweza kuchanganya mtu akadhaniwa kuwa ana Malaria
- Kuweka makao
-
- Hiki ni kipind cha kutengeneza mayai na mayai yanafika kwenye utumbo na kibofu cha mkojo
- Baadhi ya mayai anatoboa tishu mpaka kuingia kwenye kibofu na utumbo ili kutolewa na mkojo au kinyesi
- Mayai ambayo hayakuweza kutoboa yanabakiwa na yanabebwa kwenye damu mpaka kwenye ini na mapafu
- Baadhi ya mayai ambayo hayajaweza kuvuka yanasababisha mwitikio wa uvimbe kwenye utumbo na kibofu
- Mwitikio huu wa uvimbe, unasababisha makavu, na dalili nyingine za kichocho
- Ishara za kuvimba utumbo mpnana na kuhara damu na maumivu ya tumbo kwa maambukizi ya mansoni. Kutokojoa mkojo wa mwisho wenye damu na maumivu wakati wa kukojoa kama ni s. haematobium
- Hatua za mwisho
-
- Hii ni hatua ya makovu, inayotokana na uwepo wa mayai kwenye tishu. Karibu na kibofu cha mkojo hii inaweza kusababisha
- Kuziba kwa njia ya mkojo na kusababisha mkojo usitoke nje
- Kupanuka kwa njia ya mkojo (hydroureters) na kuharibika kwa figo (hydronephrosis) kunakowea kusababisha figo kufeli
- Kukakamaa kwa kibofu cha mkojo kuwa kama mfupa
- Ndani ya ini, kama mshipa wa vena ya portal utaziba, shinikizo la damu litaongezeka na kusababisha wengu/bandama kuvimba na upungufu wa damu na kuvuja damu kwenye
- Kwenye mapafu, makovu yanawea kusababisha ongezeko la shinikizo kwenye mapafu na kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi
Utambuzi
- Kuwepo kwa mayai kwenye kinyesi au mkojo
Matibabu
Praziquantel na oxamniquine ndio dawa zinazopendelewa zaidi Afrika
Kuzuia
- Tibu wagonjwa
- Kuondoa maji kwenye madimbwi
- Kuondoa nyasi na mimea kwenye sehemu za maji ili konokono wakose chakula na makazi
- Kunyoosha na kuongeza urefu wa kingo za maji
- Kutoa elimu kwa umma kuhusu namna kichocho kinavyoambukizwa na namna ya kuzuia
- Matumizi sahihi ya choo
- Epuka kuogelea kwenye madimbwi yenye maambukizi
- Vaa viatu (boots) zilizotengenezwa na mpira ili kuepuka kugusa maji yenye mabuu