Maelezo ya jumla

Kifaduro ‘’pertusis /whooping cough’’ ni aina ya maambukizi makali ya bakteria ambayo yaliwapata sana watoto kabla ya enzi za chanjo. Siku 7 – 21 baada ya kupata maambukizi, mtoto huanza kupata homa na dalili kama za mafua. Baadae mtoto huanza kupata kikohozi na kupata mkoroto unapiga kelele kali ‘’whoop’’ wakati wa kuvuta hewa ndani. Kikohozi kinaweza kuwa kikali zaidi wakati wa usiku hadi kusababisha kutapika. Ugonjwa huu ni hatari hasa kwa watoto wachanga.

Kama una kifaduro mwone daktari kama

Panga kumwona daktari haraka kama unahisi mtoto ana kifaduro. Ni vizuri kutafuta msaada wa kitabibu  kama;

  • Mtoto anaanza kusinziasinzia, anapata degedege, au kupaliwa
  • Mtoto anapata shida kupumua, au midomo au ulimi unaanza kubadilika kuwa bluu wakati wa kukohoa

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kama una kifaduro

Kifaduro ni ugonjwa unaotia wasiwasi sana, fuata taratibu zifuatazo ili kumpunguzia karaha mtoto anayeumwa.kifaduro

  • Usiwe na papara, tulia na mtulize mtoto. Kama mtoto anapata shida kulala, gawaneni majukumu ya kumhudumia usiku
  • Mpatie vinywaji kwa wingi. Jaribu kutumia asali na limao, lakini usiwapatie asali watoto wenye umri chini ya miaka 1.
    • Asali na limao husaidia kupooza koo na kupunguza maumivu ya koo. Tumia limao ambayo umeikamua, asali na maji moto.
  • Mpatie mtoto dawa ya kupunguza maumivu, kupunguza homa na kupunguza karaha. Usimpatie dawa za kupooza kikohozi – hazisaidii
    • Dawa za kupunguza maumivu husaidia kupunguza maumivu ya kichwa na misuli. Tumia ‘’acetaminophen’’ au ‘’ibuprofen’’
  • Ongeza unyevunyevu ndani ya chumba alichomo mgonjwa, itasaidia kupunguza kukohoa
    • Kuongeza unyevunyevu chumbani husaidia kupooza na kupunguza usumbufu kwenye njia ya hewa na kulainisha kamasi
    • Unaweza kuweka kifaa cha kuongeza unyevunyevu ‘’humidifier’’ chini ya kitanda cha mtoto anayeumwa au unaweza kuning’iniza taulo lenye maji kwenye ‘’radiator’’ AU.
    • Unaweza kujifukiza na mwanao kwa kukaa kwenye bafu lenye maji ya moto yanayotiririka ili kutengeneza mvuke.
  • Mpatie mtoto vyakula laini, ambavyo ni rahisi kumeza, kidogo kidogo ili kuzuia kutapika
  • Ondoa na epuka kuleta vitu vinavyoongeza usumbufu kwenye njia ya hewa ndani ya nyumba , kama vile moshi wa tumbaku na marashi makali

Kuzuia ugonjwa wa kifaduro

Kuna chanjo nzuri inayofanya kazi vizuri ya kuzuia kifaduro na imejumuishwa katika mpango wa chanjo ya watoto kitaifa. Hakikisha kuwa mtoto amechanjwa kulingana na ratiba iliyowekwa.
Angalia pia: Ratiba ya chanjo kwa watoto Tanzania

Mwone daktari kama:

Ukiwa na kifaduro panga kumwona daktari kama:

  • Unaona hali ya mtoto inazidi kuwa mbaya zaidi
  • Unahitaji kujua kama mtoto yuko tayari kiafya kurudi shuleni; Anaweza kuendelea kukohoa mara kadhaa kwa muda wa miezi kadhaa baada ya kuugua.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001561.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *