Ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa kwa wanaume ni nini?

Ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa (osteoporosis) ni hali inayosababisha mifupa ya mwili kuwa dhaifu (mifupa dhaifu) na kuongeza uwezekano wa kuvunjika. Wanaume walio na umri zaidi ya mika 70 wako kwenye hatari zaidi ya kuwa na tatizo hili.

Nani yuko kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa?

Uko kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa kama una mzazi au ndugu mwenye tatizo hili. Sababu nyingine zinazoongeza hatari ni pamoja na mlo mbaya, kuwa na uzito mdogo, kuvuta sigara, ulevi wa pombe uliopindukia, na kuwa na kiwango kidogo cha homoni ya testosteroni. Kutumia baadhi ya dawa kama vile steroids, zinaweza kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kudhoofika mifupa.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa?

Dalili hujumuisha kuvunjika mifupa, kupungua kwa uzito wa mwili, kujipinda mgongo, na maumivu ya mgongo. Kwa kawaida huwa hakuna dalili nyingine katika hatua za mwanzo  za ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa.

Ungonjwa wa kudhoofika kwa mifupa unatambuliwaje?

Daktari atakufanyia uchunguzi na kukuuliza kuhusu dalili ulizonazo. Unaweza kuhitaji kufanyiwa kipimo cha DEXA scan, kipimo hiki kinapima kuangalia unene wa mifupa.

Ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa unazuiliwa vipi?

Kama unapenda kuzuia mchakato kwa kutokea kwa ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa, ni vizuri kuacha kuvuta sigara na kunywa si zaidi ya vinywaji viwili vya pombe kwa siku. Fanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha mifupa. Kama haupati madini ya kalsiamu ya kutosha na vitamin D kuzuia tatizo hili, daktari atakuandikia virutubisho.

Kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini ya kalsiamu kama vile maziwa, bidhaa za maziwa, mbogamboga, dagaa na korosho. Wengi wetu tunapata vitamin D ya kutosha kwa kukaa angalau dakika 10 mpaka 15 kwenye mwanga wa jua, mara mbili au tatu kwa wiki.

Ugonjwa huu unatibiwaje?

Baadhi ya dawa zinaweza kupunguza uwezekano wa kuvunjika mifupa kwa wanaume wenye ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa. Dawa hizi pia zinaweza kusaidia kuzuia ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa kwa watu wanaotumia dawa za steroid kwa muda mrefu (awa za steroid husababisha mifupa kuwa dhaifu). Kuongezekwa homoni ya testosteroni kama una kiwango kidogo mwilini.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/osteoporosis.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *