Kuharibika kwa ini (sirosisi)?

Kuharibika kwa ini (sirosisi) ni hali ya ini kupata makovu yanayosababisha ini lishindwe kufanya kazi yake.

Ni nini husababisha kuharibika kwa ini (sirosisi)

Homa ya ini na ulevi wa pombe uliopindukia ndio sababu zinazoongoza kwa kusababisha shida hii. Kula mlo wenye mafuta mengi, baadhi ya dawa, na hata kinga ya mwili wenyewe inaweza kuharibu ini lako.

Ini linafanya kazi gani?

Ini linasaidia kumeng’enya chakula inachokula; kutengeneza nyongo. Ini linasaidia kuondoa sumu  kwenye damu na kutengenza protini muhimu zinazohitajika kwa shughuli nyingi za mwili, kama vile kuzuia damu kuganda ndani ya mwili.

Je ini lililoharibika linaweza kurejeshwa kwenye hali yake?

Inategemea limeharibika kwa kiwango gani, ini linaweza kujirejesha kama halijaharibiwa sana. Kama ini lako haliwezi kujirejesha katika hali yake, daktari anaweza kupendekeza ufanyiwe upasuaji wa kupandikiziwa ini jingine kutoka kwa mfadhili (transplant)

Nitajuaje kama ni tatizo la kuharibika kwa ini (sirosisi)

Daktari atafanya vipimo vya damu na uchunguzi wa mwili. Wakati mwingine kipimo cha ultrasound kitatumika kupiga picha ya ini. Daktari pia anaweza kupendekeza kuchukua sampuli kidogo ya tishu za ini ili kuzichunguza – utaratibu huu unaitwa biopsy.

Kuharibika kwa ini (sirosisi) husababisha matatizo gani?sirosisi

Ngozi inaweza kubadilika rangi na kuwa ya njano na unaweza kuvimba miguu na maeneo ya kiuno. Baadhi ya wagonjwa wanapata tatizo la kuvimba kwa mishipa / vena za damu miguuni. Unaweza kutapika damu, au unaweza kupata kinyesi chenye damu. Kutapika damu nyingi au kuwa na damu nyingi kwenye kinyesi ni dharura, na unapaswa kutafuta msaada wa kimatibabu haraka.

Baadhi ya wagonjwa wanaweza kuchanganyikiwa, na hatimaye kuingia kwenye koma. Kuchanganyikiwa kunaweza kudhibitiwa na dawa, lakini wagonjwa walichanganyikiwa hawapaswi kuendesha.

Kwa baadhi ya nyakati, matatizo yanayosababisha kuharibika kwa ini (sirosisi) yanaweza pia kuongeza uwezekano wa kupata saratani ya ini, kwa hiyo , daktari atakufanyia vipimo ili kuhakikisha hauna kansa.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000255.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *