Malengelenge sehemu za siri
Malengelenge sehemu za siri (aina ya I na II (Herpes simplex 1&2)) – Aina ya I mara nyingi hutokea mdomoni; licha ya hivyo aina zote mbili ya I na II huweza pia kuathiri kwenye njia ya viungo vya uzazi. Aina ya Pili, hujulikana kama malengelenge ya viungo vya uzazi, na ni hatari zaidi.
Jinsi malengelenge sehemu za siri yanavyoambukizwa
Kufanya ngono. Huambukiza wakati muathirika hajaanza kuonyesha dalili na wala hajui kama ana virusi. Virusi hujazana eneo hilo ambalo uambukizo ulianzia.
Dalili za malengelenge sehemu za siri
Dalili za Mwanzo: mara nyingi siku ya 2-10; dalili zinaweza kurudia rudia kuonekana, mara nyingi katika miezi ya 3-12.
Hakuna hata mmoja kati ya watu wote walioambukizwa. Kishada cha vidonda vyenye maumivu makali sana kwenye eneo la viungo vya uzazi. Maumivu wakati wa kukojoa, kutokwa na uchafu, kutokwa na mitoki, homa, maumivu ya mwili.
Mara nyingi dalili hurudia rudia kutokea katika mahali ambapo virusi waliingia kwa mara ya kwanza kwenye mwili. Hutokea zaidi kama katika hatua ya mwanzo madhara yalikuwa makubwa na yalisababishwa na ugonjwa huu aina ya II. Hatua zinazojirudia mara nyingi hazina madhara makubwa; na huchochewa na shinikizo au kupungua kwa mvutano. Ila kwa baadhi ya watu dalili kamwe haziwarudii.
Vipimo na matibabu vya malengelenge sehemu za siri
Uchunguzi wa kuangalia kwa macho na uchunguzi wa sampuli za majimaji ya malengelelenge unaofanywa maabara. Vipimo vipya vya damu vinaweza kugundua aina ya I na aina ya II. Dawa za kinga dhidi ya hivi virusi (vidonge) huweza kupunguza dalili na kushambuliwa mara kwa mara.
Madhara ya ugonjwa wa malengelenge sehemu za siri
Mtu anaweza kuishi maisha yake yote na uambukizo huu. Dalili hutofautiana kwa kila mtu. Huweza kusababisha mfadhaiko wa kihisia na kimwili pia. Pamoja na kusindwa kutoa haja ndogo, lakini watu wengi hukabiliana vizuri na hiyo hali. Vikundi vya msaada vinapatikana.
Huweza kumuambukiza mtoto wakati wa kujifungua (huzidiwa sana). Wengi huweza kuwaambukiza watoto wachanga kama mama alipata uambukizo karibu na wakati wa kuifungua. Ni asilimia moja tu ya wanawake wanao rudiwa rudiwa na haya magonjwa huwaambukiza watoto wao. Ili kuepuka kumuambukiza mtoto mama hujifungua kwa upasuaji mkubwa ili mtoto asigusane na malengelenge ya kwenye uke
MAELEZO ZAIDI KUHUSU UGONJWA WA MALENGELENGE SEHEMU ZA SIRI
Maelezo ya jumla
Ni maambukizi ya virusi yanayosababisha malengelenge, baadae yanapona na kuondoa na yana tabia ya kuja na kuondoka.
Sababu malengelenge sehemu za siri
Herpes simplex virus (HSv) aina 2
Epidemiolojia ya malengelenge sehemu za siri
Unatokea dunia nzima. Ugonjwa wa malengelenge sehemu za siri kwa kawaida huanza baada ya kushiriki ngono na ni nadra sana kabla ya kubalehe, isipokuwa kama mtoto amenyanyaswa kingono. Unapatikana zaidi (60% ya visa) katika maeneo yenye uchumi duni na kwa watu wenye wapenzi wengi.
Muda kabla dalili kuanza
Siku 2-12
Muda wa uambukizo wa malengelenge sehemu za siri
Wagonjwa wenye vidonda kwenye sehemu za siri wanaweza kuambukiza wengine kwa siku 7-12, ugonjwa ukijirudia unadumu kwa siku 4 mpaka wiki. Kuamka kwa ugonjwa wa malengelenge kwenye sehemu za siri kunatokea mara kwa amra kwa zaidi ya wanawake 50%.
Nani yuko kwenye hatari
Watu wote wapo kwenye hatari
Dalili za malengelenge sehemu za siri
- Katika tukio la kwanza la kupata dalili za malengelenge sehemu za siri – zinaanza na homa, maumivu ya kichwa, uchovu na maumivu ya misuli
- Maumivu, kuwashwa, maumivu wakati wa kukojoa na kutoa uchafu, na mtoki wenye maumivu unatokea
- Kunatokea malengelenge yaliyotawanyika mbalimbali kwenye sehemu ya juu ya via vya uzazi; malengelenge yanaweza kuwa na maji ndani, usaha, au vidonda vinavyouuma sana
- Mlango wa kizazi na njia ya mkojo inapata shida kwa 80% ya wanawake katika tukio la kwanza la ugonjwa.
- Kutoa majimaji yasiyonarngi na kuhisi maumivu wakati wa kukojoa ni dalili maalumu ya kuonesha njia ya mkojo imeathiriwa
- Kwa mara chache maambukizi yanaweza kupanda na kuathiri mfuko wa uzazi na mirija ya uzazi kwa wanawake na tezi dume kwa wanaume
Matibabu ya malengelenge sehemu za siri
Dawa ya kumeza ya acyclovir
Kuzuia
Matumizi sahihi ya kondomu ni muhimu katika kuzuia maambukizi