Ugonjwa wa mdudu kwenye kidole (uvimbe wa kucha)

Ugonjwa wa mdudu kwenye kidole (paronychia) ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa tishu zinazouzunguka ukucha. Ni tatizo linalowapata watu wengi, linaathiri tishu zinazozunguka vidole vya mikono au miguu. Kuna aina mbili za ugonjwa wa mdudu kwenye kidole; ugonjwa unaotokea haraka na ugonjwa sugu unaodumu kwa muda mrefu.

Ugonjwa wa mdudu kwenye kidole unaotokea haraka unatokana na maambukzi yanayoshambulia haraka tishu zinazozunguka ukucha. Ugonjwa sugu wa mdudu kwenye kidole unadumu kwa muda mrefu, zaidi ya wiki sita.

Ugonjwa huu unasababishwa na kemikali zinazoingia ndani ya tishu zinazouzunguka ukucha baada ya ulinzi wa kawaida wa ngozi kuharibika

Nani anapatwa na ugonjwa wa mdudu kwenye kidole?

Watu ambao wanaloweka mikono yao kwenye maji kwa muda mrefu wako kwenye hatari zaidi. Hii ni pamoja na watu wanosafisha nyumba au ofisi, wanaofua nguo, wanapika chakula, wapishi, wanaoosha vyombo, manesi na waogeleaji.

Watu wenye ugonjwa kisukari na wanaotumia aina fulani za dawa (kwa mfano za UKIMWI) pia wako kwenye hatari.

Nitajuaje kama nina ugonjwa wa mdudu wa kidole?

Baadhi ya dalili za ugonjwa wa mdudu kwenye kidole ni pamoja na:

  • Wekundu
  • Maumivu na uvimbe
  • Kuna majimaji chini ya ngozi inayozunguka ukucha
  • Ukucha unakuwa mnene na uliobadilika rangi

Ugonjwa wa mdudu kwenye kidole unatibiwa vipi?

Daktari atakuambua ni aina gani ya dawa inakufaa. Anaweza kukuambia utumie dawa ya kupaka au ya kumeza. Kama una ugonjwa mkali sana wa mdudu kwenye kidole, unaweza kuhitaji kufanyiwa upasuaji ili kuondoa maambukizi na kusaidia tishu zinazozunguka ukucha kupona.

Niatarajie nini kama nina ugonjwa wa mdudu kwenye kidole?

Ugonjwa wa mdudu kwenye kidole unaokuja haraka unaisha baada ya siku chache baada ya matibabu. Ugonjwa sugu wa mdudu kwenye kidole unaweza kuchukua wiki kadhaa mpaka miezi ili kupona na kuisha kabisa. Endelea kutumia dawa mpaka daktari atakapokuambia kuacha kutumia.

Nifanye nini ili kuzuia ugonjwa wa mdudu kwenye kidole?

Yafuatayo ni mambo unayoweza kufanya ili kuzuia kupata ugonjwa wa mdudu kwenye kidole:

  • Epuka kuweka mikono ndani ya maji au kemikali kawa muda mrefu
  • Tumia au paka mafuta au lotion kila baada ya kunawa mikono
  • Vaa mipira/glavu ili kukinga mikono unapoiweka kwenye maji au kemikali
  • Usinyonye vidole vyako
  • Epuka kuumia kwenye kucha (kama vile kutengeneza kucha, kung’ata kucha, kuweka kucha bandia)

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001444.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *