Maelezo ya jumla
Ugonjwa wa minyoo ya askaris ni maambukizi ya minyoo inayokaa kwenye utumbo mwembamba na kwa kawaida inasababisha dalili kidogo sana au haisababishi dalili kabisa
Sababu ya minyoo ya ascaris
Ascaris lumbricoides
Epidemiolojia ya minyoo ya ascaris
Ni kimelea anayepata watu wazidi kuliko wengine katika maeneo yenye usafi duni. Watoto wa shule (miaka 5-10) wanaathiriwa zaidi.
Muda kabla ya dalili kuanza
Wiki 4-8
Muda wa uambukizo ya minyoo ya ascaris
Uwezo wa kuambukiza utaendelea kuwepo kama minyoo wa kike wataendelea kuwepo. Kwa kawaida mnyoo unaweza kuishi kwa miezi 12.
Nani yuko kwenye hatari
- Watu wote wanawea kuambukizwa
- Namna ya uambukizo – life cycle
-
- Kula mayai (egg) kutoka kwenye chakula au mikono iliyochafuliwa
- Mayai yanaanguliwa yanapofika tumboni na kutoa buu (larva). Buu anatoboa ukuta wa utumbo na kusafiri kupita kwenye ini mpaka kwenye mapafu
- Buu anapita mpaka kwenye umio la hewa/koo na kishwa kumezwa kwenda tumboni
- Buu anakuwa na kutengeneza mnyoo kwenye utumbo mdogo
- Mnyoo unatengeneza mayai yanayotolewa kwenye kinyesi tayari kwa kuambukiza
Dalili za minyoo ya ascaris
- Maambukizi mengi hayasababishi dalili yoyote na mtu anaweza asijue mpaka atakapoona mnyoo mkubwa kwenye kinyesi na kwa mara chache kwenye pua au mdomo
- Buu (larva) linapokuwa likisafiri mwilini linaweza kusababisha kuwashwa, kukorota na shida kupumua, homa, kukohoa makohozi ya damu kunaweza kutokea.
- Maumivu ya tumbo yanaweza kutokea kama minyoo itasababisha kuziba kwa utumbo au mirija ya kupitisha nyongo au vimeng’enya vingine.
- Matatizo makubwa yanayoweza kusababishwa na minyoo hii ni kuziba kwa utumbo kwa sababu ya kujifunga au minyoo iliyofungamana
Utambuzi wa ugonjwa wa minyoo ya ascaris
- Kutambua mayai kwenye kinyesi kwa kutumia darubini
- Kuona minyoo mikubwa ikitoka kwenye mkundu, mdomo au pua
Matibabu y minyoo ya ascaris
Dawa zinazotumiwa kutibu ni pamoja na Albendazole au Mebendazole au Piperazine au Lavamisole
Kuzuia minyoo ya ascaris
- Tibu wagonjwa
- Matumizi sahihi ya vyoo
- Zuia mchanga wa maeneo wanayocheza watoto usichafuliwe na kinyesi
- Zingatia usafi binafsi (kunawa mikono)