Maelezo ya jumla
Ugonjwa wa minyoo ya guinea (dracunculiasis) ni maambukizi a mnyoo mkubwa unaoharibu ngozi na tishu nyingine za mwili
Sababu ugonjwa wa minyooo ya guinea
Dracunculus medinensis ni mnyoo ulio katika kundi la nematode
Epidemiolojia gounjwa wa minyoo ya guinea
Katika afrika unapatikana katika nchi 16 kusini mwa jangwa la sahara na katika Asia ni India na Yemen. Katika baadhi ya maeneo, wakazi wote wameambukizwa na katika maeneo mengini ni watu wachache tu, hasa vijana.
Umbukizo wa ugonjwa wa minyo ya guinea
Mabuu (larvae) yanazaliwa na mnyoo wa kike kwenye maji na kumezwa na kaa wa wanaitwa crutacean copepods. Ndani ya wiki 2 mabuu wakua na kukomaa tayari kwa kuambukiza. Mtu anaambukizwa baada ya kumeza hawa kaa wenye mabuu anapokuwa anakunywa maji kwenye madimbwi au visima. Wanapofika tumboni mabuu wanatoboa ukuta wa tumbo na kuingia kwenye viungo na kuanza kukua kuwa minyoo wakubwa. Minyoo wa kike wanakua wakubwa na baadae wanasafiri kutoka ndani kurudi kurudi juu karibu na ngozi (hasa kwenye miguu)
Muda kabla dalili hazijaanza
Kama miezi 12
Nani yuko kwenye hatari
Mtu yeyote anaweza kuambukizwa. Hakuna mtu mwenye kinga dhidi ya ugonjwa huu. Mtu anaweza kuambukizwa mara nyingi na maambukizi yanaweza kujirudiarudia
Dalili za ugonjwa wa minyoo ya guinea
- Kunakuwepo na dalili chache au hakuna dalili kabisa mpaka malengelenge yanapoanza kujitokeza.
- Homa na dalili za mzio zinaweza kuwepo, kama kuvimba kope, kukorota, na kuwashwa
- Mnyoo unapotoboa ngozi unaambatana na maumivu na kuvimba
- Malengelenge yanapopasuka, mnyoo unatoa majimaji yenye mabuu (larvae) na hii inasababisha kupata nafuu kidogo
- Kidonda kinachotokea kuzunguka mnyoo kinapona baada ya wiki hadi mwezi
Utambuzi wa ugonjwa wa minyooo ya guinea
- Kwa kuangalia dalili na epidemiolojia
Matibabu ya ugonjwa wa minyoo ya guinea
- Kwa kuuvuta mnyoo taratibu ili kuutoa, unafunga kwenye kijiti sehemu ya mnyoo iliyojitokeza na kuvilingisha huku kuvuta taratibu kila siku – hii ni jia inayopendelewa zaidi. Minyoo wanaweza pia kuondolewa kwa upasuaji.
- Kupatiwa dawa ya thiabendazole au metronidazole unasaidia kupunguza maumivu lakini hakuna Ushahidi kuwa zinaweza kuua minyoo.
Kuzuia ugonjwa wa minyoo ya guinea
- Toa elimu katika maeneo yenye ugonjwa huu kuhusu mambo yafutayo
-
- Ugonjwa huu unatokana na kunywa maji yenye maambukizi
- Wanakiji wenye malengelenge na vidonda wasiende karibu na vyanzo vya maji na
- Maji ya kunywa yanapaswa kuchujwa kwa kutumia chujio la nguo ili kuondoa kaa wenye mabuu
- Toa njia bora ya kupata maji safi na salama