Ugonjwa wa misuli ya moyo ni nini?

Ugonjwa wa misuli ya moyo (cardiomyopathy) ni hali inayoathiri misuli ya moyo na inaweza kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi. Mara nyingi unasababishwa na matatizo ya kurithi (kijenetiki), lakini linaweza pia kusababishwa na matatizo ya mfumo wa kinga ya mwili kama vile ugonjwa wa lupus, maambukizi, baadhi ya dawa, ugonjwa wa kisukari, matatizo ya tezi dundumio, ulevi wa pombe uliopindukia, au hata msongo mkali wa mawazo, mfano unaosababishwa na kifo cha mpendwa. Wakati mwingine, shida hii inaweza kutokea katika kipindi cha mwisho cha ujauzito au katika miezi michache baada ya kujifungua, lakini ni nadra.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa moyo?maumivu ya kifya

Dalili zinaweza kufanana na zile za moyo unaposhindwa kufanya kazi. Unaweza kupata shida kupumua, kuhisi uchovu na kukosa nguvu, kukohoa, unahisi kukosa hewa ukiwa umelala chini, kuvimba (miguu na tumbo), maumivu ya kifua, na kupoteza fahamu.

Nitajuaje kama nina ugonjwa wa misuli ya moyo?

Kama una dalili yoyote kati ya hizi nilizotaja hapa, ni vizuri kufanyiwa uchunguzi. Daktari atauliza historia yako binafsi na ya familia yako na atakufanyia uchunguzi wa mwili. Anaweza pia kufanya vipimo kadhaa ili kuangalia moyo na damu.

Ni muhimu kumwambia daktari kama kuna mtu katika familia yako na ugonjwa wa moyo, hii ni kwa sababu baadhi ya magonjwa haya yanatokea kwa wanafamilia. Daktari anaweza kuagiza ufanyiwe vipimo ili kuangalia kama uko kwenye hatari.

Ugonjwa wa misuli ya moyo unatibiwaje?mshtuko wa moyo

Matibabu yanategemea sababu ya ugonjwa wa misuli ya moyo na dalili ulizonazo. Dawa za kudhibiti shinikizo la damu au dawa za kudhibiti mapigo ya moyo zinaweza kusaidia.

Kama unavuta sigara au unakunywa pombe, unapaswa kuacha. Unapaswa kula chumv isiyozidi 2400g kwa siku. Fanya mzoezi, unapaswa kuoana na daktari kwanza kabla ya kuanza kufanya mazoezi.

Kama moyo umeanza kushindwa kufanya kazi, unaweza kuhitajika kufanyiwa upasuaji ili kuweka kifaa kidogo kwenye moyo (pacemaker) ili kuusaidia kupiga vizuri. Unaweza kuhitaji kupandikiziwa moyo mwingine kutoka kwa mfadhili kama moyo umeharibika sana. Kupandikiza moyo ni utaratibu unafanyika kwa nadra. Daktari bingwa wa moyo atakuaidia kuamua.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001105.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *