Maelezo ya jumla

Mkanda wa jeshi ‘’shingles’’ ni ugonjwa unaotokana na kuamka kwa virusi walio bakia mwilini baada ya kuugua ugonjwa wa tetekuwanga utotoni. Virusi hawa wa tetekuwanga hubakia wakiwa waejificha mwilini na baadae kujitokeza tena kinga ya mwili inapopungua. Eneo lililoathirika huanza kuuma au kuwasha na baadae kufuatiwa na upele wenye malengelenge. Unaweza pia kupatwa na homa au maumivu ya kichwa. Malengelenge baada ya muda hupasuka, kukauka na hatimae kupona kabisa baada ya wiki kadhaa, lakinu maumivu kwenye eneo hilo hubakia kwa miezi kadhaa. Ugonjwa huu unawapata zaidi wazee. Uwezekano wa kupatwa na mkanda wa jeshi huongezeka zaidi kama una upungufu wa kinga ya mwili uliotokana na kuugua kwa muda mrefu, msongo wa mawazo wa muda mrefu, UKIMWI, au kukaa sana kwenye mwanga wa jua. Hauwezi kupata mkanda wa jeshi kwa kukutana au kuguswa na mtu mwenye tetekuwanga.

Ukiwa na mkanda wa jeshi mwone daktari;

Panga kumwona daktari ili atambue kwa hakika kama ugonjwa ulio nao ni mkanda wa jeshi. Kama mkanda wa jeshi umetokea karibu sana na jicho mwone daktari haraka.

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe ukiwa na mkanda wa jeshimkanda wa jeshi

Tumia njia zifuaazo ukiwa nyumbani ili kupunguza karaha na kujihisi vizuri zaidi;

  • Itasaida kupona araka kama utapumzika kadri inavyowezekana
  • Unapokuwa na homa kunywa maji mengi
  • Tumia dawa za kupunguza maumivu ili kupunguza maumivu ya mwili, maumivu ya kichwa na homa
    • Dawa za kupunguza maumivu zitapunguza homa a maumivu, tumia ‘’acetaminophen’’, ‘’aspirin’’ au ‘’ibuprofen’’
    • Muulize mfamasia ni ipi inakufaa zaidi
  • Unaweza pia kutumia kitambaa kilicholowekwa kwenye maji ya barafu. Ukiweka kitambaa hiki kwenye eneo lililoathirika, kinaweza kupunguza maumivu na kuwashwa.
  • Kama una malengelenge kwenye mwili, oga maji ya uvuguvugu angalau mara 2-3 kila siku. Unaweza kuongeza ‘’baking soda’’ kwenye maji unayooga ili kupooza ngozi. Osha malengelenge yaliyo usoni kwa kutumia sabuni taratibu.
    • ‘’baking soda’’ inaweza kusaidia kupunguza mwasho. Ongeza vijiko 4 (hii ni sawa na kikombe kimoja) kwenye maji ya kuoga.
  • Epuka kukutana au kugusana na mtu mwingine ngozi kwa ngozi mpaka malengelenge yatakapokauka. Ni vizuri zaid kuepuka kabisa kukutana kabisa na mtu ambaye hajawahi kuugua tetekuwanga, kwa sababu unaweza kumuambukiza.

Kuzuia mkanda wa jeshi

Unaweza kuzuia kupata mkanda wa jeshi, hasa kama uko kwenye hatari au kama unapata ugonjwa huu mara kwa mara. Jaribu kufanya yafuatayo:

  • Kama unapata msongo wa mawazo mara kwa mara (na unadhani msongo unasababisha kupata mkanda wa jeshi), unaweza kujaribu kufanya mazoezi ya upumuaji na kufanya mazoezi ya kulegeza misuli ‘’musle relaxaio technique’’ ili kukusaidia. Bonyeza hapa kuifunza zaidi kuhusu njia hizi
  • Kuwa makini unapokwenda kwenye jua kali, jikinge

Mwone daktari

Ni vizuri kumwona daktari kama:

  • Malengelenge yanaanza kujaa usaha na kusambaa
  • Unapata maumivu makali sana ya kichwa au kutapika
  • Dawa za maumivu zinashindwa kudhibiti maumivu, au maumivu yanaendelea kuwepo hata baada ya malengelenge kuondoka

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000858.htm

Shares:
2 Comments
  • Zamili Shula
    Zamili Shula
    November 9, 2022 at 9:57 am

    Je! Tiba ya huu ugonjwa *mkanda wa jeshi* Ni dawa gani? Kama ipo mtu anaweza pona kabsa na huu ugonjwa usimrudie Tena?

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      November 9, 2022 at 5:23 pm

      ugonjwa wa mkanda wa jeshi unasababishwa na virusi na huwapata zaidi watu wenye upungufu wa kinga ya mwili- wenye Ukimwi, magonjwa ya kudumu yanayopunguza kinga ya mwili kama kisukari, magonjwa figo, ini au mengine kama hayo.

      zipo dawa za kudhibiti virusi kama Acyclovir zinasaidia sana kwa ajili ya kupona lakini huwa ni muhimu kurudisha kinga ya mwili katika hali yake ili ugonjwa usijirudie, hii inamaanisha kutibu sababu iliyosababisha kinga kushuka.

      Mkanda wa jeshi ni ugonjwa nyemelezi, kinga ikiwa sawa si rahisi kuupata, lakini kwa baadhi ya watu wanaweza kuupata bila kuwa na ugonjwa wowote pia

      Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *