Maelezo ya jumla
Ugonjwa wa pangusa (Chancroid) ni maambukizi ya bakteria yanayoshambulia sehemu za siri na kusababisha kidonda au vidonda vinavyouma vinavyochimba kwenda ndani.
Sababu ya ugonjwa wa pangusa
Haemophilus ducreyi
Epidemiolojia ya ugonjwa wa pangusa
Unapatikana katika nchi nyingi. Ni moja ya sababu ya vidonda sehemu za siri iliyozoeleka katika nchi nyingi. Unatambuliwa zaidi kwa wanaume, hasa wanaokutana na wanawake wanaojiuza.
Uambukizo wa ugonjwa wa pangusa
Kwa njia ya ngono, kwa kugusa moja kwa moja kidonda na usaha unaotoka kwenye mtoki. Wanaume mara nyingi hawaambukizi ugonjwa zaidi kwa sababu vidonda huwa vinauma sana.
Muda kabla dalili kuanza
Kuanzia siku 3 mpaka 5, mpaka siku 14 baada ya maambukizi
Muda wa uambukizo wa ugonjwa wa pangusa
Mgonjwa anaweza kuendelea kuambukiza mpaka atakapopona. Kadri vidonda na mtoki vikiendelea kutoa usaha wenye bakteria ataendelea kuambukiza, hii inaweza kudumu kwa wiki kadhaa au miezi kama hatapata matibabu. H. ducrei na vidonda hupona baada ya wiki 1-2.
Nani yuko kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa pangusa
Watu wote wako kwenye hatari. Watu ambao hawajatahiriwa wako kwenye hatari zaidi kuliko walioahiriwa. Hakuna Ushahidi kuwa mtu anaweza kubakia na kinga baada ya kuambukizwa.
Dalili za ugonjwa wa pangusa
- Kidonda cha kawaida cha pangusa huanza kama upele unaouma na baadae kupakuna na kuwa kidinda baada ya masaa 24
- Kidonda kinauma, kina umbo lisilosawia na kina kingo zinazoonekana wazi.
- Karibu 50% ya wanaume watapata angalau kidonda kimoja katika maisha yao
Utambuzi wa ugonjwa wa pangusa
- Kwa kuangalia dalili, lakini hakikisha sio kaswende
- Kwa kuangalia sampuli ya usaha kwenye darubini – Gram stain -typical rods in chain
- Kupandikiza sampuli – culture
Matibabu
Tibu ugonjwa wa kaswende, pangusa, & (ugonjwa wa malengelenge II)
- Penicillin 2.4 MU i. m stat ½ in each buttock +
- Azithromycin 1g PO start +
- Acyclovir 400 mg PO 8 hourly for 7 days
- Co- trimorazele AU
- Erythromycin AU
- Tetracycline
N.B. Usitoboe tezi zilizovimba (mtoki) hata kama unaona zimeiva na zina usaha ndani, zitapona kabisa baada ya matibabu
Kuzuia
- Tibu wagonjwa
- Toa vipimo kwa wenzi wa mgonjwa na toa matibabu
- Kuosha vizuri via ya uzazi kwa sabuni na maji baada ya ngono kunasaidia kupunguza maambukizi
- Kudhibiti magonjwa ya ngono kwa watu wanaojiuza
- Elimu kuhusu ngono salama ni muhimu kwa makundi yaliyo kwenye hatari