Ugonjwa wa Parkinson ni nini?

Ugonjwa wa Parkinson ni ugonjwa wa ubongo unaowaathiri zaidi wazee. Unatokea kwa sababu sehemu za ubongo zinazoongoza na kudhibiti mjongeo wa misuli umeharibiwa. Ugonjwa huu unaweza kusababisha hali ya kutetemeka na kukakamaa, kunakoweza kusababisha ukajongea kwa shida.

Nani anapata ugonjwa wa Parkinson na nini kinausababisha?

Mtu mmoja katu ya watu 100 wenye umri zaidi ya mika 60 watapata ugonjwa wa Parkinson. Hatujui kwa uhakika ni nini kinasababisha ugonjwa huu. Haumbukizwi, na kwa kawaida haurithiwi kutoka kwa wazazi au kusambaa kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto. Kama ukipata ugonjwa wa Parkinson baada ya miaka 50, hakuna ongezeko lolote la hatari kuwa watoto wako watapata ugonjwa huu pia. Hatari ya kupata ugonjwa huu kwa watoto  wa mgonjwa wa parkinson inafanana na ya wale ambao wazazi wao hawana ugonjwa huu.

Dalili za ugonjwa wa Parkinson ni zipi?

Dalili ya kwanza inayoonekana kwa watu wengi huwa ni kutetemeka viganja vya mikono. Mara nyingi hali ya mitetemo inakuwa mbaya zaidi katika upande mmoja. Watu wengi wanaona mitetemo hii wakati wakiwa wamekaa na kutulia, lakini inaondoka au kupungua kama wanatembea au kufanya kazi. Baadhi ya wagonjwa wataanza kujongea u kutembea taratibu au misuli inakakamaa kuliko kawaida. Watu wengi wanapata matatizo ya balance na ugumu kutembea.

Daktari atatambua vipi kama nina ugonjwa wa Parkinson?

Daktari atazungumza nawe na kukuchunguza mwili. Kama daktari hatokuwa na uhakika kama una ugonjwa Parkinson, anaweza kupendekeza uonane na daktari bingwa wa mfumo wa fahamu – neurologist. Kwa sababu kuutambua ugonjwa huu inweza kuwa ngumu, hasa katika hatua za mwanzo, daktari atapitia dalili zako na kukuchunguza tena ili kuhakikisha utambuzi haujakosewa katika miadi mingi inayofuata.

Ugonjwa wa parkinsoni unatibiwa vipi?

Hakuna matibabu yanayohitajika kama ugonjwa uko katika hatua za mwanzo. Dalili zinapoanza kukuzuia kufanya shughuli zako za kila siku kikamilifu, daktari ataongea na wewe kuhusu aina mbali mbali za matibabu. Zipo baadhi ya dawa zinazoweza kusaidia watu wenye ugonjwa wa Parkinson ulio katika hatua za mwanzo. Daktari atazungumza na wewe ili kukusaidia kuamua ni aina gani ya dawa ni bora kwako.

Kadri ugonjwa unapoendelea kuwa mbaya, baadhi ya watu wataanza kupata ugumu kutembea na hata kufanya shughuli mbalimbali, hata kama wanatumia dawa. Daktari anaweza kupendekeza dawa zaidi ili kusaidia kudhibiti dalili zako. Daktari anaweza pia kupendekea mazoezi ya viungo, mazoezi ya kufanya kazi na tiba shufaa, na tiba ya maongezi ili kukusaidia uendelee kuishi maisha bora kadri inavyowezekana.

Watu wengine kadri muda unavyokwenda dalili zitaendelea kuwa mbaya kiasi kwamba dawa hazitasaidia kabisa. Kwa wagonjwa kama hawa, wanaweza kuwekewa kifaa maalumu kwenye ubongo kinachoshtua ubongo kinachoitwa deep brain stimulator ili kudhibiti dalili.

Japo ugonjwa wa Parkinson hautibiki na kupona, kuna matibabu yanayoweza kukusaidia wewe na familia yako mkaishi maisha bora kadri inavyowezekana.

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000755.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *