Ugonjwa wa PID (Pelvic inflammatory disease) ni nini?

Ugonjwa wa PID (Pelvic inflammatory disease) ni maambukizi yanayowapata wanawake wengi, yanayotokea kwenye viungo vya ndani vilivyopo kwenye nyonga ya mwanamke. Kwa kawaida, ugonjwa huu unaanzia ukeni na kwenye mlango wa shingo ya kizazi, na kusambaa kwenda kwenye mji wa mimba/kizazi (uterasi), mirija ya uzazi na ovari/mayai. Wanawake wengi wenye ugonjwa wa PID wana miaka kati ya 15 na 29 ya umri.

Unawezaje kupata ugonjwa wa PID?

Ugonjwa wa PID kwa kawaida unasababishwa na bakteria kama vile klamidia na kisonono. Wanawake wengi wanapata ugonjwa wa PID kwa kushiriki ngono na mtu mwenye maambukizi, hata kama atakuwa hajui kama ameambukizwa. Kuwa na wapenzi wengi inaweza kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa PID. Wakati mwingine ugonjwa wa PID unaweza kutokana na matatizo yanayotokea baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye nyonga.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa PID?

Dalili zinaweza kuwa za kadri au kuwa kali sana. Zinajumuisha:

Unapaswa kumwona daktari kama una moja ya dalili hizi. Wakati mwingine dalili za ugonjwa wa PID zinafanana na zile za ugonjwa wa kibole (appendicitis), uvimbe kwenye ovari (ovarian cyst), maambukizi kwenye njia ya mkojo (yutiyai), au matatizo ya ukuta wa mji wa mimba. Baadhi ya wanawake hawana dalili kabisa.

Ugonjwa wa PID unatambuliwa vipi?

Daktari atafanya uchunguzi wa nyonga na kukupima kama una magonjwa ya ngono kama vile kisonono na klamidia. Vipimo hivi vinaweza kuwa vya mkojo au damu. Kwa kawaida hautahitaji vipimo vyovyote vingine.

Je, ugonjwa wa PID unatibiwaje?

Daktari atakuandikia dawa za antibiotiki. Wagonjwa wengi hawahitaji kulazwa hospitalini, isipokuwa walio wajawazito au wanojihisi kuumwa sana. Baadhi ya wanawake huhitaji kufanyiwa upasuaji kwa sababu ya matatizo yanayosababishwa na ugonjwa wa PID, lakini hii ni nadra sana.

Unapaswa kupumzika, kunywa maji ya kutosha, na epuka kudhiriki ngono mpaka utakapomaliza dawa na dalili kuisha kabisa. Ni muhimu kutumia dawa zote na kuzimaliza kama ulivyoelekezwa na daktari.

Ni nini kinaweza kutokea usipotibiwa?

Kama usipoibiwa, unaweza kubakia kupata maumivu ya nyonga kwa muda mrefu /sugu. Unaweza pia kuwa na makovu kwenye mirija ya uzazi (falopio), na hii inaweza kusababisha ukawa mgumba au ukapata ujauzito unaotungwa nje ya mimba. Kwa mara chache, ugonjwa wa PID unaweza kusababisha maambukizi makali yanayoweza kusababisha jipu kwenye ovari. Na hii inaweza kutishia maisha.

Nitazuia vipi ugonjwa wa PID?

Kupimwa mara kwa mara magonjwa ya ngono kunaweza kusaida. Usifanye ngono, au hakikisha kuwa wewe na mwenzi wako mnabakia kuwa waaminifu. Tumia kondomu kila wakati unaposhiriki ngono. Kama wewe au mwenzi wako ana ugonjwa wa klamidia au kisonono, ni muhimu kuwa wote mkatibiwe. Usifanye ngono kwanza mpaka umemaliza kutumia dawa zote ulizopewa na daktari. Usijisafishe kwa kujiingizia vidole au vitu vingine ukeni kwa sababu inaongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa PID.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000888.htm

 

 

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *