Maelezo ya jumla
Ugonjwa wa rubella unaojulikana pia kama surua ya ujerumani ‘’German measles’’ ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi. Ugonjwa huu umekua adimu sana siku hizi kwa sababu ya chanjo inayotolewa kukinga ugonjwa huu utotoni. Kwa kawaida husababisha upele mwekundu unaosambaa usoni na kisha kuenea mwili mzima.
Mara nyingi ugonjwa huu hausababishi dalili yoyote. Mtoto anaweza kuanza kupata homa ya kawaida, kuvimba kwa tezi na kutokwa na makamasi siku 2 – 3 baada ya kuambukizwa. Watu wazima wanaweza kupata maumivu ya kichwa na maumivu ya viungo. Tatizo kubwa zaidi linaloweza kusababishwa na ugonjwa wa huu ni kwa mama mjamzito. Ugonjwa huu unaweza kuleta athari mbaya kwa mtoto aliye tumboni, hasa akiambukizwa katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito.
Kama una ugonjwa wa rubella mwone daktari kama;
Panga kumwona daktari kama unadhani kuwa una ugonjwa wa rubella. Fanya vipimo unapofika ofisini kwa daktari ili kuzuia kumwambukiza mama mjamzito.
Mwone daktari haraka sana kama:
- Una ujauzito na unadhani umekutana na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa wa rubella
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kama una ugonjwa wa rubella
Kama utapata dalili, huwa ni ndogo sana na hazisababisi usumbufu wowote na mara nyingi hauhitaji matibabu yoyote. Upele hauwashi na huanza kuondoka au kupotea wenyewe baada ya siku kadhaa
- Tumia dawa za kupunguza maumivu ili kupunguza homa, kupunguza maumivu ya kichwa na maumivu ya viungo
- Dawa za maumivu husaidia kupunguza homa na kupunguza maumivu ya kichwa na maumivu ya viungo
- Kwa mtoto, mpatie ‘’acetaminophen’’ au ‘’ibuprofen’’. Hakikisha unamuuliza mfamasia ili apendekekze bidhaa inayomfaa mtoto wako.
- Watu wazima wanaweza kutumia ‘’acetaminophen’’ au ‘’ibuprofen’’.
Kuzuia ugonjwa wa rubella
Pata chanjo ya kukukinga dhidi ya ugonjwa wa huu kama ilivyoelekezwa kwenye mpango wa chanjo wa taifa. MMR (Measles, mumps, rubella) ni chanjo inayokinga dhidi ya ugonjwa wa rubella.
- Hakikisha kuwa mtoto amepata chanjo ya kumkinga dhidi ya ugonjwa wa huu kama ilivyopendekezwa na mpango wa chanjo wa taifa
- Ukipata maambukiz ya ugonjwa wa rubella hukuacha ukiwa na kinga, lakini kama unapanga kuwa mjamzito ni vizuri kupimwa kungalia kama una kinga ya kutosha hata kama ulishawahi kuugua rubella. Hakikisha kuwa umepata chanjo ya kukukinga dhidi ya ugonjwa wa rubella, ikiwezekana kabla ya kupata ujauzito.
Angalia pia: Ratiba ya chanjo kwa watoto Tanzania
Mwone daktari
Panga kumwona daktari kama:
- Unapata maumivu ya kichwa au unahisi kizunguzungu au kusinziasinzia
- Unapata maumivu ya viungo au maumivu ya macho