Maelezo ya jumla
Ugonjwa wa safura ni ugonjwa sugu unaosababishwa na maambukizi ya vimelea na kusababisha dalili mbalimbali na kiasi fulani cha upungufu wa damu.
Sababu za ugonjwa wa safura
- Ancylostoma duodenale
- Necator americanus
Epidemiolojia ya ugonjwa wa safura
Unapatikana zaidi katika nchi za kitropiki zenye usafi duni na zenye mifumo isiyobora ya kuchakata kinyesi na unyevu wa mchanga na joto linalochangua ukuaji wa mabuu yanaweza kuambukiza watu.
Uambukizo wa ugonjwa wa safura
Buu/kiluwiluwi anatoboa ngozi na kuingia ndani
Muda kabla ya kuanza kuona dalili
Dalili zinaweza kutokea baada ya wiki kadhaa au baada ya miezi kadhaa kulingana na kiasi cha maambukizi na kiwango cha madini ya chuma mtu anayotumia
Muda wa uambukizo wa ugonjwa wa safura
Watu wenye ugonjwa wanaweza kuendelea kuchafua mazingira kwa miaka mingi kama hawatapata matibabu
Nani yuko kwenye hatari zaidi
Watu wote wako kwenye hatari. Hakuna Ushahidi wowote kuwa mtu anapata kinga dhidi ya maambukizi
- Namna ya uambukizo – life cycle
-
- Kiluwiluwi (filarform larva) anatoboa ngozi na kuingia ndani, mf; kwenye miguu
- Kiluwiluwi anasafiri mpaka kwenye mapafu. anafika kwenye umio la hewa na kisha kumezwa.
- Anakua na kuwa mnyoo kwenye utumbo mdogo (mnyoo unajishikiza kwenye ukuta wa utumbo na kunyonya damu)
- Mayai (egg) yanatengenezwa na kutolewa kwenye kinyesi
- Mayai yakifika kwenye mazingira; yanaanguliwa na kutoa buu mdogo (Rhabidiform larva). Anayeendela kula na kukua kwenye mchanga
- Buu anakua na kuwa kuluwiluwi anayeweza kuambukiza baada ya wiki 1
- Kuluwiluwi anabakia kwenye udongo tayari kumwambukiza mtu mwingine
Dalili
- Kusafiri kwa kiluwiluwi ndani ya ngozi
-
- husababisha upele unaombatana na kuwashwa – hasa sehemu alipoingilia
- Kusafiri kwa kiluwiluwi kwenye mapafu
- Kunyonya kwa damu
-
- Kama ni maambukizi mepesi – hakuna dalili
- Kwa maambukizi makubwa – unaweza kupata dalili za vidonda vya tumbo kama vile maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo. kama ataendelea kupoteza damu anaweza kupungukiwa damu – unaweza kupata shida kupumua, uchovu na kizunguzungu
Utambuzi
Kuwepo kwa mayai kwenye kinyesi
Matibabu
Dawa ya Mebendazole au Albendazole au Levamisole
Kuzuia
- Matumizi sahihi ya choo
- Kuvaa viatu
- Kutibu wagonjwa