Ugonjwa wa trakoma ni nini?
Ugonjwa wa trakoma ni ugonjwa wa macho unaosababishwa na bakteria, ambao wanasababisha kope kukua kwa kwenda ndani, kuwashwa kwenye jicho, maumivu na hatimaye upofu. Maambukizi yanasambaa kupitia mawasiliano ya moja kwa moja (kupitia mikono, nguo, na shuka) na wadudu warukao ambao wamegusa maji maji kutoka katika macho au pua za mtu aliyeambukizwa. Ugonjwa huu ndio kiini kikuu kinachosababisha upofu unaoweza kuzuilika.
Ugonjwa wa trakoma husambazwaje?
Ugonjwa wa trakoma husababishwa na uchafu na vimelea, pia ugonjwa wa trakoma inaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia uhusiano wa karibu hususani kwa kutumia vitu vilivyochafuliwa kutokana na ugonjwa huu.
Ugonjwa wa trakoma huambukizwa haswa wakati kitu kimegusa jicho lililoathirika na baadaye kugusa jicho ambalo halija athirika, kwa mfano:
- Taweli, vitambaa vya mkono na karatasi ya chooni
- Vidole
- Nzi
Dalili za ugonjwa wa trakoma
Ugonjwa wa trakoma ni ungonjwa unaosabishwa na vimelea na hatimaye kusababisha upofu na huambukizwa kwa mikono michafu, nguo na nzi ambao hubeba vimelea hivyo. Mwanzoni baada ya kuambukizwa ugonjwa wa trakoma huwa haina dalili, baadae maambukizi husababisha:
- Muwasho kwenye macho
- Macho kuwa mekundu na
- Kutoa usaha kwenye macho.
- Kuathiriwa na mwangaza mkali kwenye macho.
Ugonjwa wa trakoma huathiri zaidi jamii maskini, wanaoshi katika misongamano na wanaoishi bila maji safi. Jamii zinazoishi maeneo kame na kavu pia huathirika pakubwa. Ili kuzuia maambukizi kunawa uso ni muhimu (kunawa uso kwa maji safi hupunguza usaha kutoka kwenye macho na hivyo kupunguza uwezekano wa kuwaambukiza wengine na nzi pia), mazingira safi na uwepo wa maji safi pia hupunguza maambukizi.
Upofu wa macho unaweza kuzuiwa, kama usafi wa mazingira umetiliwa maanani na jamii yote. Pia unaweza kuzuiwa kwa kutumia maji safi, kunawa nyuso na sabuni na pia mikono. Utafiti unaonyesha kuwa, kupunguza kunya/kujisaidia mahali ambapo hakuna vyoo ni muhimu katika kupunguza maambukizi haya ya ugonjwa wa trakoma na kipindupindu.
Ni muhimu kwa jamii zinazokabiliwa na maambukizi kufahamu jinsi ya kujikinga kutokana na maambukizi haya. Ni muhimu pia kuzitia moyo jamii zilizoathirika kutafuta huduma za matibabu kwa nja ya dawa ama upasuaji kabla ya kupofuka macho.
Tutawezaje sitisha/komesha Ugonjwa wa trakoma?
Kusambaa kwa ugonjwa wa trakoma kunaweza komeshwa kwa kufanya mambo mbali mbali.
- Baadhi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa trakoma kwa muda mrefu wanaweza fanyiwa upasuaji ili kurekebisha macho yao yaliyoharibiwa.
- Baadhi ya watu walioambukizwa na vimelea hivyo wapate dawa ili kuuwa vimelea vya ugonjwa wa trakoma – antibiotiki
- Kuweka uso kuwa msafi ili kuzuia nzi kubeba viini hivyo kutoka kwenye macho.
- Kuimarisha usafi wa shule na nyumba, na matumizi ya vyoo, unaeweza punguza nzi karibu nyumbani na hatimaye kupunguza uwezekano wa kupata viini vinavyosababisha ugonjwa wa trakoma.
Angalizo
Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhus shida hii.